Habari rafiki?

Moja ya mapinduzi ambayo tunayashuhudia kwenye zama hizi tunazoishi ni mapinduzi ya taarifa. Mtandao wa intaneti umerahisisha kila kitu kwa jinsi tunavyokijua. Kwanza umefanya maarifa na taarifa kusambaa kwa haraka na urahisi zaidi.

Chochote unachotaka kujua sasa hivi, popote ulipo, unaweza kuingia kwenye mtandao wa google na ukatafuta. Tena huenda umeijua AMKA MTANZANIA wakati unatafuta vitu vyako kwenye google, labda kuhusu biashara au mafanikio.

Mitandao ya kijamii, imekuwa chachu kubwa zaidi kwenye usambaaji wa taarifa na maarifa. Mitandao hii ya kijamii imerahisisha sana mawasiliano na imekuwa moja ya njia inayotengeneza mahusiano baina ya watu.

Lakini pia, kila chenye faida, kimekuwa hakikosi hasara na changamoto zake. Pamoja na wingi huu wa maarifa na taarifa, watu wamezidi kuwa wajinga, watu hawajui tena vitu, watu hawawezi tena kujifunza kwa kusoma vitu vigumu na vyenye maana. Watu hawawezi tena kukaa chini na kusoma vitabu, badala yake wanataka kusoma vitu vilivyoorodheshwa na kuondoka wakiamini wana maarifa ya kutosha.

Mitandao

Na kwa upande wa kujenga mahusiano, japo mahusiano kwenye mitandao ya kijamii yanaonekana bora, mahusiano halisi yanashuka. Mtu anaweza kuwa na marafiki elfu 5 kwenye mtandao wa kijamii, lakini hajuani na watu hata 100 ambao wanaweza kukutana na kushirikiana kwa karibu zaidi.

Hivyo haya ni mambo mawili muhimu sana kuzingatia kwenye matumizi ya mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kwa ujumla. Wingi wa maarifa yasiyo na maana, na wingi wa mahusiano yasiyo na faida. Hivyo kila unapotumia mitandao hii, angalia namna gani unahakikisha unajiepusha na matatizo hayo mawili.

Na unachoweza kufanya ni kuhakikisha unapata muda wa kupata maarifa sahihi, mfano kutenga muda na kusoma vitabu. Pia hakikisha unapata muda w akujenga mahusiano halisi. Usifurahishwe tu na ‘followers’ au ‘likes’ unazopata kwenye mitandao hii.

NIMEONDOKA KWENYE MITANDAO YOTE YA KIJAMII.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha marafiki zangu wote kwamba nimeondoka kwenye mitandao yote ya kijamii niliyokuwa natumia hapo awali. Hivyo kwa wale ambao walikuwa wananifuatilia kupitia mitandao hii, mtakuwa mmeona ghafla sionekani tena kwenye mitandao hii. Nimeondoka kabisa kwenye mitandao hii, na sina mpango wa kurejea huko kwa siku za karibuni.

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0

Kwa nini nimeondoka kwenye mitandao hii?

Kama nilivyotangulia kusema, mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa sana. kazi zangu zimeweza kuwafikia wengi kupitia mitandao hii. Najua wengi sana wamenijua kupitia mitandao ya kijamii, ambapo bila hiyo leo wasingenijua na kunufaika na huduma ninazotoa, pamoja na kununua huduma ninazouza pia.

Lakini nimefikia maamuzi haya baada ya kufanya tathmini na kugundua muda ninaotumia kuhudumia watu kwenye mitandao hiyo haulingani na huduma ninayotoa. Kwamba kama nikiondoa muda huo na kuuweka kwenye kuandaa kazi bora zaidi, watu wananufaika zaidi.

Mwaka huu 2018 ulipoanza, niliacha kabisa kutumia mitandao hii, lakini sikuondoa akaunti zangu. Nilifanya kama jaribio la kuona maamuzi hayo yatakuwa na madhara gani kwa kazi zangu. Nilichojifunza ni kwamba nisipoweka muda wangu kwenye mitandao na maeneo mengine, napata muda zaidi wa kujifunza na kufanya mawasiliano yenye maana na wengine.

Hivyo nimeondoka kwenye mitandao hii, ili kuweka nguvu na muda zaidi kwenye kazi ninazofanya, za kuandaa maarifa bora zaidi kwa wale ambao wananufaika nayo.

SEHEMU MBILI PEKEE NINAZOPATIKANA KWENYE MTANDAO WA INTANETI.

Nimeondoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini sijaondoka kwenye mtandao wa intaneti kabisa. Sehemu kubwa ya kipato changu inatokana na mtandao wa intaneti.

Hivyo zipo sehemu mbili pekee nitakazokuwa napatikana kwenye mtandao wa intaneti.

Sehemu ya kwanza ni kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA, www.amkamtanzania.com ambapo kila siku nitakuwa nakushirikisha makala mbalimbali ambazo zitakuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Mtandao huu ni bure kabisa na una makala nyingi za kujifunza.

vitabu softcopy

Sehemu ya pili ni mtandao wa KISIMA CHA MAARIFA, www.kisimachamaaarifa.co.tz huu ni mtandao maalumu kwa wale waliojitoa kuhakikisha wanafanikiwa. Hapa ni kwa wale ambao wameshaondoka kwenye kutamani kufanikiwa na wamefika kwenye hatua ya kwamba lazima wafanikiwe na hivyo kuwa tayari kufanya chochote wanachohitajika kufanya ili kufanikiwa. Mtandao huu ni wa kulipia ada kwa mwaka, ambapo utapata kusoma makala na kuwa kwenye kundi la wasap ambapo utapata madarasa mbalimbali kwa ajili ya mafanikio zaidi.

Ili kupata nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ujumbe kwa njia ya WASAP kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA. Msisitizo, ujumbe unatuma kwa njia ya wasap na siyo ujumbe wa kawaida.

OMBI LANGU KWAKO RAFIKI YANGU.

Nina ombi moja kwako rafiki yangu, na ombi hili ni kuwaalika watu zaidi kufuatilia huduma ninazotoa. Najua wapo watu wengi sana ambao hawajajua uwepo wa huduma ninazotoa, lakini wewe unajua na unawajua. Hivyo naomba uwe balozi wangu, waambie watu watembelee mtandao wa AMKA MTANZANIA, www.amkamtanzania.com kujifunza.

Kama umesoma makala nzuri kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA, au umepokea kupitia email, basi watumie wengine unaowajua ili wajifunze.

Kama kuna mtu unamjua ambaye anapitia changamoto mbalimbali kwenye maisha yake, mshauri atembelee AMKA MTANZANIA kuna makala nyingi za kujifunza.

Nakutegemea sana wewe rafiki yangu tuweze kuwafikia wengi zaidi. Kama huduma ambazo nimekuwa natoa zimekuwa na manufaa kwenye maisha yako, basi waalike na wengine pia wajifunze.

Nikushukuru sana rafiki yangu kwa namna tumeendelea kuwa pamoja, na ninaendelea kukuahidi kwamba nitaendelea kukushirikisha maarifa bora kabisa, ya kukuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Usomaji