Siku ya kwanza kwa mtu kufanya chochote kile, huwa anaifanya kwa kujali sana, anaweka juhudi kubwa katika kufanya na hiyo inamletea matokeo bora sana.
Lakini sasa yanakuja mazoea, baada ya muda mtu anazoea kile anachofanya, anazoea matokeo ambayo amekuwa anapata na anaanza kupata matokeo ambayo siyo makubwa tena.
Kwa matokeo kuendelea kuwa vile vile kunamfanya mtu kukata tamaa na kuona hakuna namna ya kupiga hatua zaidi.

Unachohitaji kwenye hali kama hiyo ni kufanya kwa kujali zaidi. Chochote ambacho unafanya kwa mazoea, anza kukifanya kwa kujali zaidi. Fanya kama vile ndiyo siku ya kwanza, fanya kama vile kila mtu anakuona.
SOMA; #UKURASA WA 1031; Jinsi Ya Kuwa Sumaku Ya Fedha….
Fanya kitu kwa uasili wake, kifanye kiwe na nembo yako, kifanye kiwe chenye thamani zaidi.
Kwa kifupi fanya kwa sababu unaweza na unataka kufanya na siyo kwa sababu inabidi ufanye. Ikishakuwa ni kubidi, utafanya kwa mazoea, lakini ikiwa ni kutaka, utafanya kwa ubora zaidi.
Utatakaje kufanya kitu halafu ukifanye hovyo, ukifanye kwa mazoea?
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog