“The good life is one inspired by love and guided by knowledge,” – Bertrand Russell
Ni siki nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni fursa bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HAMASA NA MWONGOZO WA MAISHA BORA…
Kila mtu anapenda kuwa ma maisha bora,
Lakini wengi sana hawajui nini kinaleta maisha bora.
Wengi wanaishia kutamani lakini hawayapati maisha hayo bora.
Maisha bora yanatengenezwa ma vitu viwili;
Cha kwanza ni HAMASA YA UPENDO,
Upendo ndiyo hamasa kuu ya maisha bora.
Unapaswa kujipenda wewe mwenyewe, ndiyo uweze kuchukua hatua bora sana kwa ajili yako.
Unapaswa kuwapenda wale wanaokuzunguka, ili uweze kufanya mazuri kwa ajili yao.
Na muhimu zaidi unapaswa kupenda sana kile unachofanya ndiyo uweze kukifanya kwa kujituma sana.
Kitu cha pili kinachotengeneza maisha bora ni MWONGOZO WA MAARIFA.
Maarifa ndiyo mwongozo mkuu wa maisha bora.
Lazima ujue ni nini hasa unataka kufanya na maisha yako, kisha ujue kwa undani kuhusu kile unachotaka.
Lazima ujifunze sana kuhusiana na watu na kuhusiana na mazingira yanayokuzunguka.
Unahitaji kuwa na maarifa juu ya maisha ya mafanikio na maisha bora kwa ujumla.
Kujifunza kila siku na kila mara ni hitaji muhimu la maisha bora na ya mafanikio makubwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kuhamasika kwa UPENDO na kuongozwa na MAARIFA.
#UpendoHamasa #MaarifaMwongozo #Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha