Rafiki yangu mpendwa,

Tunapitia wakati ambao umekuwa na changamoto nyingi sana.

Kwanza kabisa, kwa wengi, hasa wale waliopata elimu mpaka ya juu, wanaona kama walidanganywa maisha yao yote. Walipokuwa shule waliimbiwa sana kuhusu kusoma kwa bidii, kufaulu na kisha kupata kazi nzuri na kuwa na maisha bora.

Wakatimiza hili, wakasoma sana kwa bidii, wakafaulu vizuri, na baada ya kuhitimu ndipo ukweli ukajitokeza hadharani. Kwanza wachache ndiyo wanapata ajira, na kwa hao wachache wanaopata ajira, maisha bora bado hawajaona yanafananaje, maana ajira zimeishia kuwa kifungo kwao, wapo kwenye madeni na kipato hakiwatoshelezi. Wengine wengi hawajapata ajira na hivyo kuona kama elimu zao hazijawa na msaada kwao.

Kwa upande wa pili, wapo wale ambao hawakupata nafasi ya kufikia elimu ya juu sana. walipata elimu ya msingi au ya sekondari, na baada ya hapo wakajiingiza kwenye shughuli za uzalishaji. Hawa nao siyo kwamba wana neema kubwa sana. Maana wengi wapo kwenye shughuli za uzalishaji kwa miaka mingi na hakuna hatua wanapiga.

Michango

Hapa unakutana na mafundi ambao kwa zaidi ya miaka kumi wanafanya kazi zile zile, ambapo ikitokea ameumwa basi kazi hawezi tena kufanya. Unakutana na wafanyabiashara ambao wana bishara hiyo moja kwa zaidi ya miaka kumi, haikui wala kuendelea, na kama yeye asipokuwepo basi biashara haiwezi kwenda kabisa.

Kwa nje unaweza kuona watu hawa wana uhuru, lakini ni mpaka uingie kwenye viatu vyao ndiyo unagundua kwamba wamenasa kwenye magereza waliyoyatengeneza wao wenyewe. Hawana ule uhuru ambao wengi wanatamani wangefanya kama wao. Na siyo kwa sababu wamenyimwa uhuru huo, ila kwa sababu wamefanya makosa ya kuchimba shimo, ambalo wameingia wenyewe.

Swali langu kwako rafiki yangu, je upo katika kundi lolote kati ya hayo? Je upo kwenye kundi la wale waliosoma na kupata ajira lakini maisha ni magumu? Upo kwenye kundi la waliosoma na ajira hakuna? Upo kwenye kundi la watu waliojiajiri kwa ujuzi wao wenyewe kama ufundi lakini usipokuwepo kazi haziendi? Au upo kwenye kundi la wafanyabiashara ambao kama usipokuwepo biashara yako haiwezi kwenda?

Kama umesema ndiyo kwenye kundi lolote kati ya hayo niliyotaja, basi ninahitaji kusema na wewe, nina habari njema sana kwako, habari za kukuwezesha kutengeneza uhuru wako wa kipato, kwa kuwa na njia isiyo na ukomo ya kukuingizia kipato.

Rafiki, katika zama hizi tunazoishi, kwa namna mambo yanavyokwenda kasi, njia pekee ya kujihakikishia uhuru wa kipato ni kuwa na biashara, inayojiendesha kwa faida.

Lakini changamoto ni kwamba kila mtu anafanya biashara, na hivyo inaonekana kama ulimwengu wa bishara umeshajaa na hakuna kipya unachoweza kufanya.

Habari njema nilizonazo kwako ni kwamba, katika watu 100 wanaofanya biashara 99 siyo wafanyabiashara, bali ni wachuuzi, watu wanaopanga bidhaa au huduma zao na kama kuna yeyote anayepita akaziona na kutaka kuzinunua basi watafurahia. Kama asipojitokeza yeyote kununua basi wanasikitika kwamba mambo siyo mzuri na kusubiri tena siku nyingine.

Kwa zama tunazoishi sasa, ni hatari sana kuendesha biashara yako kwa mazoea, kuendesha biashara yako kusubiri wateja waje wenyewe, waone na kuja. Ni kweli wanaweza kuja, lakini siyo wateja bora, ni wale wateja ambao wameachwa na wafanyabiashara wajanja.

Ninataka kukufanya wewe rafiki yangu uwe mfanyabiashara mjanja, unayewaleta wateja kwenye biashara yako, wanaridhika sana na wakiondoka wanaleta wateja zaidi. Hii ndiyo maana ya biashara, na ukishajua jinsi ya kufanya hivyo, unakuwa umekata tiketi ya uhuru wa maisha yako.

Rafiki, napenda kukuambia kwamba, nimekuandalia semina ya KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50. Kwenye semina hii, utajifunza mbinu 50 za kufanyia kazi kwenye biashara yako, ambazo zitawafanya wateja waje na kuleta wateja zaidi na zaidi. Na kwa ujio wa wateja hao, utaweza kufanya mauzo zaidi ya ulivyozoea kuuza sasa na kisha kutengeneza faida zaidi.

Je ungependa kushiriki semina hii? Je ungependa kuanzisha na hata kukuza biashara unayofanya sasa iwe ya uhuru mkubwa kwako? Kama majibu ni ndiyo,  basi maelezo kamili yapo hapa;

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog