“True life is lived when tiny changes occur.” — Leo Tolstoy
Siku mpya, siku bora na siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri kwako mwanamafanikio kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana leo.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MABADILIKO MADOGO NDIYO MAISHA…
Mtoto hazaliwi leo halafu kesho akaanza kutembea na kuongea.
Bali itamchukua muda kuweza kukaa, kitambaa, kusimama na kisha kutembea, tena baada ya kuanguka anguka sana.
Ataamza kusema ma, ba baadaye mama, baba kabla hajaweza kusema sentensi kamili.
Huwa tunapenda mafanikio kwenye maisha yetu yaje kama mvua, mara moja maish yetu yawe na mabadiliko makubwa.
Lakini hivyo sivyo mambo yanavyokwenda.
Mabadiliko madogo madogo ndiyo maisha yenyewe.
Vitu vingi tunavyotaka vitatokea kidogo kidogo mpaka kufikia ile hatua ya tunachokitaka.
Hivyo mwanamafanikio, unachohitaji kufanyia kazi ni mabadiliko madogo madogo ya kila siku.
Kila siku, kazana kuwa bora zaidi kuliko siku uliyopita,
Chagua kupiga hatua zaidi ya ulivyopiga jana,
Fanya kujaribu vitu zaidi ya ulivyofanya siku iliyopita.
Kuna ambavyo utafanikiwa,
Vingine utashindwa,
Lakini kwa hakika utajifunza na kuona nafasi ya kusonga mbele zaidi.
Njia pekee ya kufikia mafanikio makubwa unayotaka kufikia kwenye maisha yako ni kupig hatua ndogo ndogo kila siku.
Na kujua kwamba mwisho wa siku, hatua ndogo ndogo unazopiga zitazalisha matokeo makubwa sana.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki,
Siku ya kupiga hatua ndogo ndogo.
#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha