Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari WAKATI SAHIHI NI SASA…
Rafiki, kuna wakati unajua kitu, ambacho hukuwa unakijua huko nyuma na unajiambia kama ningejua hichi mapema ningekuwa mbali sana.
Si kweli, huenda ulisikia kitu hicho mapema na ukakipuuzia, kwa sababu hukuwa tayari.
Wakati mwingine unajua kitu, unapata hamasa kweli ya kufanya, lakini unapotaka kuanza kufanya unajiambia huu siyo wakati sahihi.
Unajiambia bado hujawa tayari na hivyo unahitaji maandalizi zaidi.
Huhitaji maandalizi yoyote kwenye kufanya kile ambacho ni muhimu zaidi kwako, unachohitaji ni kuanza kufanya, sasa hivi.
Rafiki, wakati sahihi kwako kufanya yale muhimu zaidi kwenye maisha yako ni sasa.
Hakuna wakati mwingine mzuri kama huu,
Hakuna wakati utajiona upo tayari kwa kila kitu.
Unahitaji kuanza na unahitaji kuanza sasa.
Leo hii, nenda kapitie mipango yako yote na kwa ile muhimu zaidi, anza kufanya sasa.
Anza hata na hatua ndogo kabisa.
Kama kitu ni muhimu na unakijali, basi unachohitaji ni kuanza kufanya.
Mengine utajifunza zaidi ukishaanza kufanya kuliko ukisubiri mpaka uwe tayari.
Uwe na siku bora sana leo rafiki, siku ya kufanya yale muhimu kwa maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYoueLife
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha