Rafiki yangu mpendwa,

Mauzo ndiyo kazi ambayo kila mmoja wetu anaifanya kila siku ya maisha yake. Kila mmoja wetu kuna kitu anauza, awe ameajiriwa au yupo kwenye biashara.

Pamoja na kwamba mauzo ndiyo kitu ambacho kila mmoja wetu anafanya, watu wengi sana ni wabovu kwenye mauzo. Watu wengi hawana mbinu sahihi za mauzo na hivyo inakuwa vigumu kwao kuuza na kupiga hatua.

Changamoto kubwa kwenye mauzo ni pale mteja anapokataa kununua. Na siyo kwamba kila mteja atakuambia sitaki kununua, ila kama mteja hajasema ndiyo nanunua, basi amekataa.

Mteja anaweza kukataa kwa kukuambia kwa sasa sipo tayari, jua tu hapo kakataa ila anatafuta njia rahisi ya kuachana na wewe.

Wakati mwingine mteja atakuambia nitakutafuta, jua kabisa hapo umeshampoteza.

Lakini sasa kuna wakati mteja anakuja na sababu ambazo kweli zinakuhitaji ufikiri kwa kina na uje na majibu sahihi.

Mfano mteja anakuambia unachouza ni ghali sana, au siyo imara kama ninavyotaka, au nataka muundo mwingine/rangi nyingine.

Wateja wana kila aina ya upinzani na sababu kwa nini wasinunue, hata kama ni kitu wanachokihitaji kweli. Na kila mtu anafanya hivyo kwa sababu kutoa fedha kunauma. Hebu fikiria fedha yako uliyoitafuta kwa jasho sana, halafu uje uitoe kirahisi tu kwa sababu mtu amekuambia kuna kitu anauza!

Na hapo kumbuka ukishatoa fedha hiyo kununua kitu, huwezi tena kuitumia kwenye jambo jingine muhimu. Hivyo ili mteja aweze kuwa tayari kununua chochote unachomuuzia, lazima awe na kila sababu ya kufanya hivyo. Lazima kila aina ya upinzani atakaoleta uwe na majibu yake.

Na muhimu zaidi, lazima uwe na kitu ambacho kitamsaidia kweli, ambacho akishawishika kununua, atakushukuru kwa maisha yake yote kwa namna kitu hicho kimemsaidia.

How-to-sell-anything

Ili kuweza kuuza zaidi, ili kuweza kuondokana na vikwazo mbalimbali vya wateja, kila wakati unapokuwa unauza, kuwa tayari kufanya vitu hivi vitatu;

Moja; Kuwa Na Kitu Cha Juu Na Bora Zaidi.

Kwenye kila kitu unachouza, hakikisha una kitu cha juu yake, ambacho ni bora zaidi na pia bei yake ni ya juu zaidi. Kitu hichi utakitumia pale mteja anapokuambia kile unachotaka kumuuzia siyo imara kama anavyotaka. Na hapo unamhamishia kwenye kitu imara na bora zaidi, na ambacho bei yake ni ya juu zaidi.

Wakati mwingine wateja wanaamini kitu ni kizuri pale kinapokuwa na bei ya juu. Hivyo ukiwa na vitu vya  bei rahisi vyote, n rahisi kupoteza baadhi ya wateja ambao wanaamini bei inaendana na ubora wa kitu.

Hakikisha una kitu cha juu ambacho unaweza kumuuzia mteja anayehitaji zaidi. Wakati mwingine mteja anakuwa ameshatumia kile unachotaka kumuuzia na anahitaji cha juu zaidi. Hivyo kuwa na kitu cha juu ni njia rahisi ya kumbakisha mteja kwenye biashara yako.

Mbili; Kuwa Na Kitu Sawa, Lakini Cha Muundo, Rangi Na Mfumo Tofauti.

Kuna wakati utaona mteja anaelekea kabisa kununua, lakini anakuja na sababu kwamba muundo wa kile unachomuuzia siyo anaotaka, au rangi siyo anayopenda au mfumo wake siyo anaotaka. Hapo lazima uwe na kitu kinachoendana na hicho, chenye bei sawa, lakini kina muundi, rangi au mfumo tofauti.

Muhimu ni kumfanya mteja aone ana wigo mpana wa kuchagua na halazimiki kuchukua kile ambacho unamwambia achukue yeye. Lakini hapa pia unapaswa kuwa makini, ukiwa na machaguo mengi sana unamchelewesha mteja kufanya maamuzi na anaweza asinunue kabisa.

Unaweza kusikiliza kikwazo chake ni nini kisha ukamwambia tunaweza kukupa hicho unachotaka, au kinachokaribiana na hicho. Lengo kuu ni mteja asiwe na sababu ya kutokununua.

SOMA; Mambo Matano Ya Kuzingatia Katika Kuendesha Na Kukuza Biashara Kwenye Nyakati Ngumu Kiuchumi.

Tatu; kuwa na kitu cha chini.

Wapo wateja ambao watakuambia wanataka sana unachouza, lakini bei ni kali na hawaiwezi. Watakupa kila sababu kwa nini mambo ni magumu na bei hiyo hawaiwezi. Hapa ndipo unapohitaji kuwa na kitu kinachoendana na unachouza, lakini gharama yake ni ya chini kidogo.

Hapo unamfanya mteja akose tena sababu kwa nini hawezi kununua. Lakini pia kuwa makini hapa, kitu cha chini unachochagua kuuza kiwe na viwango vizuri na imara, isiwe kitu cha hivyo, ambacho mteja atajutia kununua.

Kwa kuwa na kitu cha chini, mara zote mteja atakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua kulingana na uwezo wake.

Hizo ndiyo njia tatu muhimu sana kuuza pele ambapo mteja anakataa kununua, angalia jinsi ya kuzitumia kwenye biashara yako ili uweze kuwauzia wateja wako zaidi.

Kabla sijamaliza, nikukumbushe haya muhimu sana;

  1. Lazima ujue hitaji hasa la mteja ni lipi, kisha kuwa na vitu ambavyo vitatimiza hitaji lake na vitajibu mapingamizi yake kwenye kununua.
  2. Hakikisha mteja anaelewa manufaa ya kile anachonunua na namna kinakwenda kutatua matatizo na changamoto zao.
  3. Kabla hujakimbilia kumpa mteja wako mbadala, hakikisha umeshajua nini hasa anataka, na kikwazo chake ni nini. Usimpe mbadala kabla hajakupa vikwazo, atatengeneza vikwazo vipya kwenye mbadala wako na utashindwa kuuza. Mfano kama hajakuambia kikwazo ni bei, na wewe ukamwambia kuna cha bei ndogo, atakuambia hata hiyo bei ndogo bado ni kubwa kwake.
  4. Japokuwa unataka kuuza, usimuuzie mteja kitu ambacho hakimfai, kama unaona anachotaka huna, mwache aende na mshauri wapi anaweza kupata kile hasa anachotaka. Kuuza kitu ambacho hakimsaidii mteja ila tu unataka kuuza jua utauza mara moja lakini hutamuuzia tena mteja huyo siku zijazo.
  5. Mteja akiondoka kwenye biashara yako awe na tabasamu, na awe tayari kuwaambia wengine nao waje kununua kwako. Hivyo mchakato mzima wa mauzo unapaswa kwenda kiurafiki kabisa kiasi kwambe mteja mwenyewe anafurahia kulipia kile unachomuuzia.

Rafiki, ninayo mengi sana nimekuandalia kuhusu kuongeza wateja na kuongeza mauzo kwenye biashara yako na hatimaye kuongeza faidia kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye biashara yako.

Na yote hayo nitakushirikisha kwenye semina ambayo tutakwenda kuifanya mwezi julai 2018. Kama bado hujapata taarifa za semina na kuchukua hatua, basi soma hapo chini, na nikushauri sana, chukua hatua mara moja.

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog