Siku mpya,
Siku bora,
Siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UNAENDA WAPI?
Mwandishi mmoja aliwahi kuandika, watu wengi hawajui wanakoenda, lakini wanaenda kwa kasi ya ajabu sana.
Wati hawajui wanachotaka, ila siku nzima wapo bize sana.
Na huu ndiyo uhalisia wa maisha,
Ndiyo namna ambavyo wengi sana wanachagua kupoteza muda wao.
Ndiyo njia bora kwa wengi kujificha, wasifanye yaliyo muhimu na kukazana na yasiyo muhimu, ili tu waonekane kuna vitu wanafanya.
Rafiki yangu, kabla hujafanya chochote, jipe sekunde tano tu za kujiuliza na kujipa jibu, wapi unaenda na maisha hako? Nini hasa unachotaka kwenye haya maisha.
Ukishapata jibu, jiulize kama unachotaka kufanya kinakufikisha unakoenda, kinakupa unachotaka kwenye maisha yako.
Una muda mchache sana, una nguvu zenye ukomo, ila unayo mengi sana ya kufanya.
Kama hutajikumbusha kila wakati, ni rahisi kusahau unakokwenda na unachotaka na kujikuta umesombwa na mafuriko ya kile ambacho kipa mtu anafanya.
Na mara nyingi sana, ukishajikuta uko kwenye kundi la wengi, jua hufanyi kitu sahihi kwako. Ni rahisi sana kumezwa na kundi kama hujikumbushi wapi unaenda na nini unataka.
Tafakari hili kila mara, unaenda wapi, unataka nini. Usiingie kwenye mkumbo wa wengi, simamia yale muhimu zaidi kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufuata njia yako, siku ya kufanya yale muhimu kwako.
#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #MudaNiSasa #WhatEverItTakes#WachaManenoWekaKazi
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha