People are effective because they say no.” — Peter Drucker

Amka mwanamafanikio,
Amka kutoka kwenye usingizi usio na mwisho,
Amka kutoka kwenye hali ya kutokuchukua hatua,
Amka kutoka kwenye hali ya kusubiri uwe tayari,
Amka kutoka kwenye kujidanganya kwa kulalamika na kuwalaumu wengine.
Kama ipo hatua yoyote unataka kupiga kwenye maisha yako, unahitaji kuchukua hatua leo, la sivyo hutachukua hatua kabisa.

Leo hii tunakwenda kuongozwa na msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UFANISI NI KUSEMA HAPANA…
Kuna tofauti kubwa sana ya kuwa bize na kuzalisha,
Kuwa bize unakuwa na shughuli nyingi za kufanya, hila ya kujali umuhimu na kipaumbele kwenye shughuli hizo. Unafajya tu ili uonekane unafanya.
Kuzalisha ni pale unapofanya kile ambacho kinaleta matokeo yanayokupeleka kule unakotaka kwenda. Kuzalisha ni pale unapofanya kitu kwa ufanisi wa hali ya juu.

Sasa rafiki yangu, watu wanapenda sana kuwa bize kuliko kuzalisha.
Wapo tayari kufanya kila kinachojitokeza mbele yao ili kujiridhisha wao na wengine pia.
Na hicho ndiyo chanzo kikuu cha wengi kushindwa.

Ili uweze kuwa na ufanisi kwenye maisha yako ni lazima uweze kusema HAPANA.
Unahitaji kusema hapana kwa vitu vizuri, ili uweze kupata vile vilivyo bora zaido.
Unahitaji kusema hapana kwa chochote ambacho hakichangii kukusogeza karibu na ndoto zako.
Unahitaji kuwa tayari kusema hapana hata kama kuna kizuri utakachopoteza, maana huwezi kupata bora kama hutapoteza kizuri.

Ufanisi na uzalishaji ni kusema hapana kwa yale yasiyo muhimu zaidi ili kupata muda na nguvu ya kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi.
Kwa chochote kipya unachotaka kufanya kwenye maisha yako, anza na HAPANA, kisha jishawishi kwa nini kitu hicho kinahitaji ndiyo. Na kama ni ndiyo basi iwe ndiyo kweli, ili uweze kuwa na ufanisi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kusema hapana kwa yale yasiyo muhimu sana ili kupata muda na nguvu kwa yale muhimu.

#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha