Rafiki yangu mpendwa,

Mwandishi Charlie “Tremendous” Jones amewahi kusema, “Five years from today, you will be the same person that you are today, except for the books you read and the people you meet.”

Akimaanisha miaka mitano kutoka sasa, utakuwa kama ulivyo leo, isipokuwa kwa vitabu ulivyosoma na watu uliokutana nao.

Hii ina maana kwamba kama hakuna vitabu vipya unavyosoma mara kwa mara, na kama hukutani na watu wapya, watu wanaotaka kupiga hatua kubwa zaidi, utaendelea kuwa hivyo ulivyo. Na kwa kuwa dunia inasonga mbele, kama unabaki kuwa ulivyo, maana yake dunia inakuacha nyuma.

Hii ndiyo sababu kila mara nimekuwa nakusisitiza sana kuhusu usomaji wa vitabu, nimekuwa nakuchambulia vitabu kama sehemu ya wewe kupata hamasa ya kuvisoma. Pia kwa wale wanaokuwa na sababu kwamba hawawezi kusoma vitabu, nimewaandalia program maalumu ya kusoma vitabu.

Na kwa eneo la pili ambalo Charlie anatusisitiza, eneo la kukutana na watu wapya, nina hakika wengi kinachotukwamisha ni wale wanaotuzunguka. Unakuta hawafikirii makubwa kama unavyofikiria wewe. Na kama unaishi kwenye jamii ambayo wamezoea ukawaida, wanaweza kukutukuza ukipata mafanikio kidogo na ukaanza kujidanganya kwamba umepiga hatua.

Lakini unapokutana na watu wenye ndoto kubwa zaidi, wanaochukua hatua kubwa zaidi unahamasika na kuona wewe bado hujapiga hatua unazopaswa kupiga. Pia unapata watu wapya wa kushirikiana nao, ambao wanakusukuma kuweza kufanikiwa zaidi.

Ili kuhakikisha hukosi watu sahihi watakaokuwezesha kupiga hatua zaidi, kila mwaka nimekuwa nakuandalia semina ya kukutana ana kwa ana, ambapo unapata nafasi ya kukutana na watu wenye kiu ya mafanikio, watu ambao wamejitoa kulipa gharama yoyote wanayopaswa kulipa ili waweze kufanikiwa. Hawa ni watu ambao kwa kuzungukwa nao tu unajisikia hamasa ya kufanya zaidi.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ambapo utapata nafasi ya kukutana na watu sahihi wa safari yako ya mafanikio. Hili ni tukio linalofanyika mara moja kwa mwaka, lakini madhara yake yanadumu kwa mwaka mzima.

Kwa kushiriki semina hii, unakuza mtandao wako kwa kuwa na watu sahihi, ambao watakuwa chanzo kikuu cha taarifa, maarifa na hamasa kwako ili kufanikiwa zaidi.

Unapokuja kwenye semina hii, jiandae kukutana na watu wengine ambao wana hasira ya mafanikio kama wewe. Na ninaweza kukuhakikishia kwamba unakwenda kukutana na watu makini kwa sababu ada ya kushiriki semina hii ni kubwa kidogo kuliko wengi walivyozoea. Hivyo atakayekuwa tayari kulipa ada hii, ni yule ambaye amejitoa kweli, ambaye haruhusu chochote kimrudishe nyuma.

Na hiyo ndiyo sababu kubwa kwa nini hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, kwa sababu ndiyo semina pekee itakayokuweka kwenye mstari sahihi wa kuelekea kwenye mafanikio makubwa zaidi.

semina 2017 4
Sehemu ya wahudhuriaji wa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

Taarifa Kamili Ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Semina yetu ya kukutana moja kwa moja, kwa wanamafanikio wote, yaani wale watu waliojitoa kupambana ili kufikia maisha ya mafanikio itafanyika siku ya jumamosi, tarehe 03/11/2018.

Itakuwa ni semina ya siku nzima, kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja usiku. Yatakuwa ni masaa 12 ya kujifunza, kushirikiana na wengine na kutengeneza mtandao mkubwa kwa ajili ya mafanikio.

Semina hii itafanyika jijini Dar es salaam, eneo itakapofanyika semina hii taarifa zitatolewa baadaye. Lakini itakuwa eneo zuri, kwenye moja ya hoteli kubwa za dar es salaam.

Mambo matano muhimu utakayonufaika nayo kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018.

MOJA; FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO; kuitumia miaka kumi ijayo kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye maisha yako.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutakwenda kujifunza na kutengeneza mkakati wa kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye maisha yako kwa miaka kumi ijayo.

Nilichojifunza ni kwamba watu wamekuwa wanaona miaka kumi ni mingi sana wanapoiangalia kwa mbele, lakini ukiiangalia kwa nyuma ni midogo sana. Watu wanaogopa kupangilia miaka 10 ijayo, lakini muda unawapita na wanajikuta wako pale pale.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutakwenda kujifunza na utafanya kwa vitendo zoezi la kutengeneza mkakati wa mafanikio makubwa ya maisha yako kwa miaka kumi ijayo.

MBILI; ONGEZA MAUZO NA FAIDA KWENYE BIASHARA YAKO.

Changamoto nyingi za biashara zinaanzia kwenye mauzo kidogo na faida ndogo zaidi. Haya ni maeneo mawili ambayo ukiyafanyia kazi, utakwenda kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye biashara yako.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA utajifunza na kutengeneza mkakati wa kwenda kuongeza mauzo na faida zaidi kwenye biashara yako. Haijalishi biashara yako ni ndogo au kubwa kiasi gani, unaweza kuongeza mauzo zaidi na faida kubwa zaidi.

Karibu kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA ujifunze hili kwa kina na uweze kuchukua hatua.

TATU; MKAKATI WA KUELEKEA KWENYE UHURU WA KIFEDHA.

Fedha ni muhimu na fedha zina changamoto nyingi. Kila mtu anapenda kuwa na fedha zaidi, lakini wengi hatuna mikakati tunayoifanyia kazi kuelekea uhuru wa kifedha. Kwa sababu haijalishi una kipato kikubwa kiasi gani, kama huna mkakati wa kufikia uhuru wa kifedha, maisha yako kifedha yataendelea kuwa magumu.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, tutajifunza mkakati muhimu wa kuelekea uhuru wa kifedha, hasa maeneo makuu mawili ambayo ni kipato na uwekezaji.

NNE; SHUHUDA ZA WALIOCHUKUA HATUA NA KUPATA MATOKEO MAZURI.

Wapo wenzetu ambao wamechukua hatua kupitia mafunzo ambayo tumekuwa tunayapata wote na wameweza kupiga hatua fulani kwenye maisha yao na hata biashara zao.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutakwenda kupata shuhuda za wenzetu hapa, wakitueleza walipotoka, walipo sasa na kule wanakoelekea. Tutapata nafasi nzuri ya kujifunza kutoka kwao, tutapata fursa ya kuwauliza maswali na kujua waliwezaje kukabiliana na changamoto mbalimbali walizokutana nazo.

TANO; KUKUZA MTANDAO WAKO WA MAFANIKIO.

Wanasema haijalishi unajua nini, bali unamjua nani. Moja ya vikwazo vikubwa kwenye mafanikio ni kukosa mtandao sahihi, wa watu unaowajua na wanaokujua.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 utapata nafasi ya kukuza mtandao wako wa mafanikio. Kwa sababu watu wanaohudhuria semina hii siyo watu wa kawaida, ni watu ambao wanayasaka mafanikio na wanajua watayafikia, hawana wasiwasi na wala hawakati tamaa.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ili uweze kukuza mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki yangu, hayo ndiyo mambo matano makubwa ambayo utaondoka nayo kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ambayo yataufanya mwaka wa mafanikio 2018/2019 ukawe mwaka bora kabisa kwako.

Utaondoka ukiwa umetengeneza mikakati utakayokwenda kufanyia kazi, ambayo itakuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Ada ya kushiriki semina hii ya kukutana moja kwa moja novemba 3 mwaka huu 2018 itakuwa tsh 100,000/= (shilingi laki moja). Ada hii itajumuisha chai ya asubuhi, chakula cha mchana, na chai ya jioni. Pia utapata kijitabu cha kuandika unayojifunza kwenye semina, kalamu ya kuandika pamoja na mwongozo uliochapwa wa mkakati unaokwenda kufanyia kazi baada ya semina.

Mwisho wa kulipa ada ili uweze kushiriki semina hii itakuwa tarehe 31 mwezi oktoba 2018.

Karibu sana kwenye semina, karibu sana uwahi kupata nafasi yako ya kushiriki semina hii kabla nafasi zilizopo hazijaisha. Tofauti na semina za mtandao, semina za kukutana moja kwa moja kuna ukomo wa watu wangapi wanaweza kuhudhuria.

Mkakati mzuri wa kulipia semina hii ili usiikose.

Semina hii ni muhimu sana kwa kila mtu ambaye anataka kupiga hatua kubwa kwenye maisha yake, hivyo hupaswi kwa namna yoyote ile kuikosa.

Najua ada ya shilingi laki moja ni kubwa kwa wengi ambao semina hii inawahusu sana. Lakini nataka semina hii iwe bora sana kwa kila atakayeshiriki, hivyo gharama za maandalizi ni kubwa pia.

Kwa kuzingatia ukubwa huu wa ada, ndiyo maana nimekupa taarifa za semina hii mapema sana ili uweze kujiandaa na usiseme umeshindwa kushiriki kwa sababu huna fedha ya kulipia.

Ada ya semina ni tsh 100,000/= kama utatoka mkoani kwa ajili ya kushiriki semina hii, ukilipa nauli ya kwenda na kurudi na malazi ya siku moja au mbili, utahitaji kiasi kingine cha fedha, kama bajeti imekubana kabisa, unaweza kujibana kwa laki moja nyingine ukasafiri na kupata malazi ya siku moja.

Hivyo basi, kama unataka kushiriki semina hii, na huwezi kulipa fedha hiyo kwa pamoja, nakupa nafasi ya kulipa kidogo kidogo, ili mpaka tarehe 31/10/2018 uwe umekamilisha ada ya semina.

Kuanzia leo mpaka tarehe ya mwisho kulipia ni siku 91, ambapo kila siku ukiweka elfu moja pembeni, labda ukapunguza kitu fulani ambacho umekuwa unafanya, basi mwisho wa kulipia utakuwa umeweza kulipa ada hiyo. kama utasafiri basi unahitaji kuweka elfu mbili mpaka tatu kwa siku.

Kuanzia leo mpaka tarehe ya mwisho kulipia kuna wiki 13, ambapo kila wiki ukiweka pembeni elfu 10 au elfu 20 kama unasafiri, utaweza kushiriki semina hii bila matata kabisa.

Na kuanzia leo mpaka tarehe ya mwisho kulipia, kuna miezi mitatu, hii ina maana kila mwisho wa mwezi ukaweka elfu 35, basi utaweza kukamilisha kulipia semina hii na ukawa na uhakika wa kushiriki.

Rafiki yangu, sitaki kumwacha hata mmoja ambaye ana nia ya dhati ya kushiriki semina hii. Hivyo chagua mpango wowote wa malipo unaotaka kufanya na nitakuwa tayari kukusaidia.

Kama utataka kutuma fedha kidogo kidogo kila siku, kila wiki au kila mwezi, nijulishe na nitapokea malipo yako kidogo kidogo na kutuza kumbukumbu zako kwa usahihi.

Karibu sana rafiki kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, semina pekee usiyopaswa kuikosa kabisa kama upo makini na maisha yako na umejitoa kufanikiwa zaidi.

Kufanya malipo ya semina, tumia namba zifuatazo za simu. Mpesa tumia 0755 953 887, tigopesa na airtel money tumia 0717 396 253, namba zote zinaonesha jina AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma malipo ya ada ya kushiriki semina, tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo, wenye majina yako kamili, namba za simu na barua pepe na sema umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Kama utahitaji kulipia kidogo kidogo tuwasiliane kwenye namba hizi ili kupanga utaratibu wa malipo yako.

Jiwekee nafasi yako ya kuhakikisha unashiriki.

Ili kutokukosa nafasi ya kushiriki semina hii, nimekuandalia kundi maalumu la wasap linalohusiana na semina hii. Karibu ujiunge na kundi hili kama upo tayari kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, ambapo nitakujumuisha kwenye mipango ya semina hii pamoja na kuandaa njia bora zaidi za kukusaidia.

Hivyo kama utashiriki semina hii, hata kama hulipii sasa, fungua kiungo hichi; https://chat.whatsapp.com/L3F4jaeYcZO4drSCxWYrPr kisha nitumie ujumbe kwa wasap namba 0717396253 wenye majina yako kamili, namba ya simu, unakoishi na shughuli unazofanya, pamoja na tarehe unayotegemea kufanya malipo ya semina.

Karibu sana rafiki yangu, karibu sana tukutane ana kwa ana, pamoja na wanamafanikio wengine tarehe 3 novemba 2018. Lengo langu kwenye semina hii ni kupata angalau dakika moja ya kuongea na kila atakayeshiriki, napenda sana kumjua kila mmoja wa anayenufaika na maarifa tunayoshirikishana kila siku.

Nikukumbushe tu rafiki;

Tarehe ya semina ni 03/11/2018,

Mahali itakapofanyika ni dar es salaam,

Mambo utakayonufaika nayo ni matano,

Ada ya kushiriki ni tsh 100,000/=,

Mwisho wa kulipa ada ili kushiriki ni tarehe 31/10/2018,

Namba za malipo ni 0755953887/ 0717396253 (AMANI MAKIRITA),

Unaweza kulipa kidogo kidogo, kwa kila siku, kila wiki au kila mwezi.

Kama una uhakika utashiriki semina hii, karibu uingie kwenye kundi maalumu la wasap la SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, bonyeza kiungo hichi ili kuingia kwenye kundi; https://chat.whatsapp.com/L3F4jaeYcZO4drSCxWYrPr

Karibu sana rafiki, karibu tuweke mikakati ya kufanyia kazi kwa mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha yetu.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha