Kama unataka kuendesha biashara yako vizuri na kama unataka kufanya mambo mazuri kwenye hii dunia, basi jua ya kwamba unahitaji kujijali wewe kwanza kabla ya vitu vingine vyovyote.
Ni kweli biashara itakuhitaji uweke juhudi kubwa, itahitaji muda wako mwingi, lakini kama hutajijali wewe mwenyewe kwanza, hutafika mbali. Utaweza kupata matokeo mazuri kwa muda mfupi, lakini hutaweza kwenda kwa muda mrefu.
Unapojijali wewe mwenyewe, kwa kutenga muda kwa ajili yako, unajijengea uwezo wa kuitumia biashara yako kuwafikia wengi zaidi. Kwa sababu huwezi kuwasaidia wengine kama huwezi kujisaidia wewe mwenyewe.
Tenga masaa machache kwenye siku yako, ambapo hayo yatakuwa kwa ajili ya mwili wako na roho yako.
Anza kuyaendesha maisha yako wewe mwenyewe kabla hata hujaanza kuendesha biashara yako. Kwa sababu kama maisha yako yana migogoro, basi jua biashara yako pia itakuwa na migogoro.
Unahitaji kuwa na ubinafsi kwako kwanza, kuhakikisha maisha yako yanasimama vizuri kwa sababu mikiki mikiki ya biashara itayumbisha sana maisha yako yasipokuwa imara.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,