Ni siki nyinyine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA MAONI YANGEKUWA SHERIA…
Kama maoni ya kila mtu yangekuwa ndiyo sheria, dunia nzima ingeshateketea na wote kufa.
Kwa sababu kila mtu ana maoni yake kwenye kila kitu.
Jambo lolote utakalochagua kufanya kwenye maisha yako, watu watakuwa na maoni tofauti.
Wapo watakaokuambia unafanya jambo sahihi na endelea.
Na pia wapo watakaokuambia unafanya makosa makubwa sana na unapaswa kuacha mara moja.
Nani atakuwa sahihi katika makundi hayo mawili?
Hakuna hata mmoja aliye sahihi, wewe pekee ndiye uliye sahihi.
Kwa sababu kila mtu anaweza kuwa na maoni yake,
Lakini kumbuka maoni ni maoni na siyo sheria.
Hivyo unapaswa kujua nini hasa unataka na maisha yako na kisha kuendea kile unachotaka.
Ukishaamua, unahitaji kuachana kabisa na maoni ya kila mtu,
Kwa sababu ukianza kusikiliza kila aina ya maoni, utachanganyikiwa na hutaweza kupiga hatua yoyote.
Hakuna maoni ambayo ni sheria, hivyo huwajibiki kufuata maoninya kila mtu.
Na maoni pekee ambayo ni muhimu na sahihi kwako ni maoni yako mwenyewe.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kwenda kuchukua hatua kubwa na kutoruhusu maoni ya kila mtu yakuvuruge.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha