Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari WAKATI MWINGINE MZURI NI SASA…
Wanasema wakati mzuri wa kupanda mti ulikuwa miaka 20 iliyopita…
Na wakati mwingine mzuri ni sasa.
Kuna wakati kwenye maisha yako unajifunza vitu au unakutana na watu na kujiambia kama ningejua haya mapema ningekuwa mbali sana.

Ni kweli huenda ungejua mapema ungekuwa mbali, lakini hukujua mapema, umejua sasa, unachofanya ni nini?
Chochote ambacho umejua sasa, na ukajiambia ungekuwa umejua mda mrefu ingekusaidia, unaweza kuanza sasa na ikakusaidia.

Kwa kifupi, chochote ambacho unatamani ungekijua muda mrefu, umeshakijua sasa, hivyo chukua hatua sasa.
Unaweza kuanza wakati wowote na unaweza kuanzia popote.
Ukishajua unachoona ni muhimu, kifanyie kazi.

Na kwa kusisitiza tu, usijidanganye kwamba umri umeenda au muda haukutoshi.
Kama kitu ni muhimu zaidi kwako anza kukifanya.
Unaweza kuanza wakati wowote kwenye maisha yako na ukapiga hatua kubwa.

Ukawe na siki bora sana ya leo, siku ya kuanza chochote muhimu unachojifunza, bila ya kujali muda gani umekijua.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha