“Many people do not gain in wisdom as they get older; they only gain in weight.”
Siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni siku tuliyoisubiri kwa hamu kubwa sana.
Siku tuliyojiambia kesho tutafanya hiki au kile.
Siku yenyewe ndiyo hii, ni wajibu wetu kwenda kuchukua hatua na kuacha kuahirisha mambo.
Siku ya leo tunakwenda kuongozwa na msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA. Kwa namna hii, tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ONGEZA BUSARA NA SIYO UZITO…
Watu wengi, kadiri umri unavyokwenda, wanaongezeka uzito na siyo busara.
Hili ni kosa kubwa na hatari kubwa kwenye maisha pia.
Kwa sababu ongezeko la uzito linaleta hatari za magonjwa,
Na kutoongezeka kwa busara, kunafanya maisha yawe magumu zaidi.
Hakikisha kila siku mpya unakuwa bora kuliko siku iliyopita,
Hakikisha kila siku kuna kitu kipya unajifunza,
Hakikisha kila siku mpya kuna hatua unazopiga ambazo hujawahi kupiga.
Kabla hujalisha mwili wako, anza kwanza kulisha akili yako.
Ukiongeza busara, hata uzito hautakuwa tatizo kwako.
Lakini kama utakazana kulisha mwili, huku akili ikiwa haina chakula, itaongeza uzito wa mwili huku akili ikiwa na utapiamlo.
Na ni heri kuwa na utapiamlo wa mwili lakini siyo wa akili.
Maana akili ikiwa na utapiamlo, yaani ikikosa maarifa sahihi, utaishia kutumiwa na wengine kwa namna wanavyotaka wao wenyewe.
Utadanganywa, utatapeliwa, utaibiwa, utatumikishwa na hayo yote ni kwa sababu hujalisha akili yako maarifa sahihi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kulisha akili yako zaidi kuliko unavyoulisha mwili.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha