Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NIDHAMU NA UHURU…
Watu wengi hufikiri NIDHAMU NA UHURU ni vitu viwili vinavyopingana, vitu ambavyo haviwezi kwenda pamoja.
Wengi wanafikiri kuwa na NIDHAMU maana yake ni kujinyima UHURU.
Wengi huchukulia UHURU ni kufanya kile unachojisikia kufanya kwa muda wowote unaojisikia kufanya, kitu ambacho ni kinyume na NIDHAMU.
Ukweli ni kwamba NIDHAMU NA UHURU ni vitu vinavyokwenda pamoja, kimoja kisipokuwepo na kingine hakiwezi kuwepo.
Kama huna NIDHAMU, huwezi kupata UHURU. Na UHURU nila ya NIDHAMU utakumaliza kabisa.
Kama unataka kuwa na uhuru zaidi, unahitaji kujenga nidhamu.
Kwa sababu nidhamu itakuwekea mipaka ya yapi muhimu kufanya na yapi ya kupuuzia.
Chukua mfano wa fedha, ili ufikie uhuru wa kifedha, unahitaji kuwa na nidhamu kubwa sana kwenye fedha.
Kama utakosa nidhamu, hata kama kipato ni kikubwa kiasi gani, utaishia kutegemea kipato maisha yako yote na hivyo kukosa uhuru wa kifedha.
Kama unapenda kuwa huru zaidi, penda nidhamu zaidi. Jijengee nidhamu ya hali ya juu sana kwenye kila eneo la maisha yako na utapata uhuru mkubwa kadiri utakavyo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea nidhamu zaidi ili kufikia uhuru zaidi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha