Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIPE RUHUSA MWENYEWE…
Kama kuna kitu unataka kufanya kwenye maisha yako, basi unapaswa kujipa ruhusa wewe mwenyewe na kukifanya.
Kama unasubiri ruhusa kutoka kwa mtu mwingine yeyote, jua kabisa hutaipata na hivyo hutafanya unachotaka kufanya.
Kama kuna kitu unataka kuanza, unapaswa kujiruhusu kuanza hata kama hujakamilika, kwa sababu ukisubiri ukamilifu, hutaanza chochote.
Kama kuna hatua unataka kupiga, unapaswa kujiruhusu kupiga hata kama hakuna anayekubaliana na wewe. Ukisubiri mpaka kila mtu akubaliane na wewe, hutapiga hatua yoyote kubwa.
Kumbuka, hakuna anayejua unachotaka kama wewe, hakuna anayejua umuhimu wake kama wewe, na hakuna mwenye msukumo wa kufanya kama ulionao wewe.
Hivyo kama msukumo upo ndani yako, fanya, mengine utajifunza kadiri unavypendelea kufanya.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujipa ruhusa ya kufanya hata kama unajiona hujawa tayari au hakuna anayekubaliana na wewe. Kile ambacho ni muhimu kabisa kwako, anza kukifanya, usisubiri ruhusa ya yeyote, jiruhusu mwenyewe.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha