“Be more concerned with your character than with your reputation. Your character is what you really are, while your reputation is merely what others think you are.” – Coach John Wooden.
AMKA Mwanamafanikio,
AMKA kwenye siku hii nyingine nzuri sana na ya kipekee kwetu.
Siku ambayo tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TABIA NA SIFA…
Kila mtu anapenda kuwa na sifa nzuri lwa wengine,
Na wengi wanachukua mpaka hatua ya kujaribu kutengeneza sifa ambayo wanataka wengine waione kwao, wanaigiza maisha ili waonekane wana sifa fulani.
Lakini sifa za aina hiyo huwa hazidumu.
Kitu pekee unachopaswa kusumbuka nacho wewe ni tabia yako, kwa sababu tabia yako ndiyo kitu unachoweza kudhibiti.
Tabia yako ndivyo ulivyo wewe.
Sifa ni kitu cha nje, kile wanachoona wengine.
Tabia ni kitu cha ndani, jinsi ulivyo wewe mwenyewe.
Hivyo kazana kujenga tabia bora, na watu watatengeneza sifa yao juu yako.
Usihangaike sana na sifa, maana huna nguvu ya kuitengeneza,
Hangaika na tabia, maana una nguvu ya kutengeneza tabia unayotaka na kupitia tabia zako, watu watatengeneza sifa yako.
Ishi maisha na siyo kuigiza maisha, ukitaka sifa, utalazimika kuigiza maisha. Lakini ukijenga tabia, hutakuwa na haja ya kuigiza maisha.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea tabia bora sana kwako ambazo zitakufikisha unakotaka kufika.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha