“Dripping water hollows out stone, not through force but through persistence.” — Ovid

Siku mpya,
Siku bora
Na siku ya kipekee sana kwetu.
Ni bahati ya kipekee sana kwetu kuweza kuiona siku hii nyingine nzuri.
Siyo kila mtu ameweza kuiona siku hii, hivyo tushukuru kwa nafasi hii.
Pia tuitumie vizuri nafasi ya leo, maana huenda hatutapata nafasi nyingine kama hii.

Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, huku tukiongozwa na TATUA, AMUA NA ONGOZA, na hivi vinatuwezesha kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NGUVU YA MATONE YA MAJI…
Kila mmoja wetu amewahi kuona maajabu ambayo yanafanywa na matone ya maji.
Matone madogo madogo yanayodondoka kwenye jiwe gumu au hata mwamba, baada ya muda yanavunja mwamba huo.
Lakini tone moja haliwezi kuvunja mwamba huo.
Hata ukikusanya matone hayo na kuyamwaga mara moja bado hayatavunja mwamba huo.

Je unajua nguvu ya kuvunja mwamba kwenye matone ya maji inatoka wapi?
Siyo kwenye maji, bali kwenye msimamo.
Kitendo cha matone kujirudia rudia bila ya kuacha ndicho kinachopelekea mwamba kuvunjika.

Kwenye maisha yako, unaweza kuitumia nguvu ya tone la maji kufanya makubwa sana.
Hatua ndogo ndogo unazochukua kila siku bila ya kuacha, zinajenga tabia kubwa ambayo itakuwezesha kufanya makubwa sana.
Hatua ndogo ndogo unazochukua kwenye kazi yako au biashara yako kila siku zinakufanya uzidi kuwa bora sana.

Na hata unapokutana na ugumu kwenye maisha yako, hatua ndogo unazoendelea kuchukua, zitakuwezesha kuangusha ugumu ule.

Kitu muhimu sana kwenye maisha yako ni kuwa na msimamo, kurudia rudia bila ya kuacha. Chagua vitu ambavyo utafanya kila siku ya maisha yako, bila ya kuacha hata siku moja.
Chagua namna ambavyo utafanya kazi au biashara yako kila siku bila ya kuacha.
Hata kama unachofanya ni kidogo na cha kawaida sana, kitendo cha kufanya kila siku bila ya kuacha, kitakuwezesha kufanya makubwa sana.

Kwa kuwa na msimamo, kwa kurudia rudia bila ya kuacha au kukata tamaa, utaweza kuvuka ugumu wowote unaokutana nao.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchukua hatua ndogo ndogo kwa msimamo bila ya kuacha.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha