Seneca said, “Things will get thrown at you and things will hit you. Life’s no soft affair.”

Siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana imeanza.
Ni siku ambayo umekuwa unaisubiria kwa hamu, siku ambayo jana ulisema kesho nita….
Kesho ya jana ndiyo tayari imeshafika hivyo nenda kachukue hatua leo.

Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, na mwongozo wetu wa mafanikio kwa mwaka huu 2018 ni TATUA, AMUA NA ONGOZA, kwa kutumia hivi tutakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari DUNIA ITAKURUSHIA VITU…
Tunatamani sana dunia ingekuwa na usawa,
Tunatamani sana mambo yangekuwa rahisi,
Tunatamani sana kama tungeweza kupata kila tunachotaka kwa namna tunavyotaka.

Lakini sivyo uhalisia wa dunia ulivyo,
Tunapanga hivi, vinatokea vingine,
Tunategemea hivi yanatokea mengine,
Na mbaya zaidi, dunia inaweka vikwazo kwenye njia zetu, inaturushia vitu ambavyo vinakuwa kikwazo kwetu kupata tunachotaka.

Usitamani dunia kwenda kama unavyotaka,
Usitamani mambo yawe rahisi kwako,
Badala yake acha dunia iende kama inavyoenda,
Kazana kuwa bora zaidi ili uweze kuvuka kila ugumu.

Kama Seneca anavyotuambia, dunia itaturushia vitu, vitu vitatuumiza na dunia haina usawa.
Kulalamikia lolote kati ya hayo ni kupoteza muda wako.
Hivyo chukua hatua ya kuwa bora badala ya kulalamika au kutaka dunia iwe kama unavyotaka wewe.

Kama dunia itakurushia mawe, badala ya kulalamikia mawe hayo, yatumie kujenga msingi imara wa mafanikio yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa bora zaidi ili usiangushwe na chochote ambacho dunia inakurushia.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha