“Fight if you must, work hard, give your best but never quit in the face of difficulty.” – Sanchita Pandey

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIKIMBIE UGUMU…
Kabla ya kupata mafanikio makubwa kwenye chochote unachofanya, lazima kwanza upitie ugumu.
Lazima ukutane na changamoto kubwa sana zinazokukatisha tamaa na kukufanya uone hakuna matumaini mbele.

Lakini kama kweli unataka kufanikiwa, basi kamwe usikate tamaa.
Kamwe usiukimbie ugumu.
Pambana kama inabidi,
Weka kazi kubwa,
Lakini usikate tamaa kabisa.
Yaani hata lile wazo tu la kukata tamaa halipaswi kupita kwenye akili yako.

Kwa sababu ukishaanza kuwa na wasiwasi kuhusu kufika unakotaka kufika, itakuwa vigumu kwako kufika.
Wewe fanya kile kilicho bora,
Usiangalie ugumj, bali angalia kipo bora zaidi unachoweza kufanya.
Na kwa kupeleka mawazo yako yote kwenye kile bora unachoweza kufanya, mawazo ya kukata tamaa yatapotea kabisa.

Rafiki, unapokutana na ugumu, usianze kufikiria huo ndiyo mwisho, badala yake ona huo ndiyo mwanzo wa kujijua zaidi, hiyo ndiyo dalili kwamba unachofanya ni sahihi kwa mafanikio makubwa.
Kwa sababu kitu kisipokuwa na ugumu, kila mtu atafanya na thamani yake inakuwa ndogo.
Ila kitu kinapokuwa kigumu, wachache pekee ndiyo wanaofanya na thamani yake inakuwa kubwa sana.

Uwe na siku bora saba ya leo rafiki, siku ya kupambana na kila aina ya ugumu unaokutana nao bila hata ya kufikiria kukata tamaa.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha