Pablo Picasso said, “Only put off until tomorrow what you are willing to die having left undone.”
Siku mpya,
Siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri kwetu sisi wanamafanikio kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana leo hii na hata siku zijazo.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KITU PEKEE UNACHORUHUSIWA KUAHIRISHA…
Kuahirisha mambo siyo kitu kibaya, pale tu unapojua ni nini unaahirisha na kwa nini unaahirisha.
Lakini kuahirisha kila kitu bila ya kujua kwa kina, ni kujiandaa kushindwa.
Kwa sababu kitu chochote ambacho unakiahirisha, una nafasi ndogo sana ya kuja kukifanya baadaye.
Kama Picasso alivyotuambia, kitu pekee unachopaswa kuahirisha ni kile ambacho upo tayari kufa na kukiacha hakijafanywa.
Kama hakuna tofauti yoyote ndani yako iwapo utafanya au hutafanya, basi hicho unaweza kuahirisha.
Lakini vitu vingine vyote, vile vitu ambavyo ni muhimu zaidi kwako, vile ambavyo hutaki kufa kabla hujavifanya, basi unapaswa kuvifanya kama ulivyopanga kufanya na kamwe usiahirishe.
Ni rahisi sana kuahirisha na kujiambia nitafanya kesho,
Tena inashawishi sana kuahirisha pale unapokutana na ugumu.
Lakini kabla hujakimbilia kuahirisha, jiulize swali hili; je nipo tayari kufa na kuacha kitu hiki hakijafanywa?
Hili ni swali muhimu sana na lenye uzito mkubwa, kwa sababu ukiahirisha chochote, nafasi ya kukifanya tena inakuwa ndogo sana.
Na kama wote tunavyojua, hatujui ni lini tutakutana na kifo, kwa sababu kinaweza kututembelea muda wowote.
Hivyo ni vyema kufanya kile tulichopanga kufanya, kwa muda tuliopanga kufanya.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kila ulichopanga kufanya bila ya kuahirisha.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha