Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FIKIRIA KILE UNACHOTAKA MARA ZOTE….
Akili yetu ina nguvu kubwa sana ya kuweza kuumba chochote kile tunachofikiri, kama kitu hicho tutakifikiria muda wote na kikatawala akili zetu.
Haijalishi ni nini unafikiri, akili yako itakuletea hicho.
Ukifikiria kile unachotaka, na ukakifikiria muda wote, akili yako itakuweka kwenye mazingira ya kuweza kukipata.
Kadhalika ukifikiria kile usichotaka na ukakifikiria kwa muda mrefu, akili yako itakuletea hicho pia.

Akili haiwezi kutofautisha hasi na chanya kwenye fikra zetu, ikiona fikra zimekaa kwa muda mrefu, inajua hizo ndiyo muhimu na kuhakikisha zinakamilika.
Hivyo rafiki, muda wote tawala akili yako kwa fikra ya kile unachotaka.
Mara zote kuwa na picha ya ndoto zako kubwa kwenye akili yako, yafikirie maono makubwa uliyonayo mara zote.

Usiruhusu fikra zinazopingana na unachotaka kuingia kwenye akili yako, hapo utaivuruga na itashindwa kukuandalia mazingira mazuri ya kile unachotaka.
Usiruhusu akili yako iwe na wasiwasi wowote juu ya unachotaka, kuwa na uhakika wa kupata chochote unachotaka na usijiwekee mashaka yoyote.
Hata kama umekosea, ondokana kabisa na wasiwasi wowote unaoweza kuingia kwenye akili yako, maana huo utakuvuruga zaidi.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kufikiria kile unachotaka na kupuuza kabisa vile vinavyopingana na unachotaka.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha