Rafiki yangu mpendwa,

Kwa zaidi ya miezi mitatu sasa nimekuwa nakupa taarifa za SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ambayo utafanyika tarehe 03/11/2018 jijini dar es salaam. Na ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kuwa umelipa ada ambapo mwisho wa kulipa ada ni leo tarehe 31/10/2018.

Nimechukua muda mrefu kukupa taarifa hizi na kukumbusha mara kwa mara kwa sababu sipendi ukose tukio hili kubwa kwa mafanikio yako ambalo linatokea mara moja pekee kwa mwaka. Na wakati naanza kukupa taarifa hizi, kulikuwa na muda wa kutosha kuweza kulipa elfu moja kila siku na ukaweza kushiriki.

Leo napenda kukufahamisha ya kwamba tumefikia siku ya mwisho kabisa ya kupata nafasi ya kushiriki semina hii. Hivyo kama hukuwa umekamilisha malipo ya kushiriki semina hii, fanya hivyo kabla ya siku ya leo kuisha.

Siku ya leo ikishaisha, hutaweza tena kupata nafasi hii ya kipekee sana. Nakusisitiza hivi rafiki yangu kwa sababu kwa uzoefu watu huwa wanakuja baada ya tarehe ya mwisho kulipa wakiomba kulipia na wanakuta nafasi hazipatikani tena.

Rafiki, ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ni tsh 100,000/= ambayo itagharamia huduma zote muhimu za siku ya semina.

Ada inalipwa kwa njia ya MPESA; 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253, majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA.

Fanya malipo yako leo hii na ukishatuma fedha, tuma ujumbe wenye majina yako na namba ya simu ili kupewa taarifa zaidi kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Kamilisha malipo yako leo hii rafiki yangu ili jumamosi tuwe pamoja, nimekuandalia vitu vingi na vizuri kwa ajili ya mwaka wa mafanikio 2018/2019.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Yafuatayo ni mambo saba muhimu sana unayopaswa kuyajua kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

  1. Hii ni semina maalumu kwa wale wote wenye kiu ya kutaka kufanikiwa zaidi. Walengwa wakuu ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ila mtu yeyote anakaribishwa kushiriki hata kama siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kinachohitajika ni mtu awe na kiu ya mafanikio na awe tayari kujifunza na kuchukua hatua ili kufanikiwa.
  2. Kama kuna mtu wako wa karibu ambaye unaona anaweza kunufaika na semina hii, unaweza kumlipia ada au kumshawishi alipe ada na ukaja naye, hata kama siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza pia kuja na mwenza wako, kuja na wafanyakazi wako na wengine wote ambao wanahusika na mafanikio yako, watakuwa na mengi ya kujifunza.
  3. Semina hii inafanyika mara moja pekee kwa mwaka, hivyo ukikosa semina hii ni mpaka tena mwaka ujao. Yale unayokwenda kujifunza utakuwa na mwongozo wa kuyafanyia kazi kwa mwaka mzima.
  4. Kutakuwa na nafasi 12 za watu nitakaofanya nao kazi kwa karibu mwaka mzima ili kukuza zaidi biashara zao. Nafasi hizi zitapatikana kwa wale watakaoshiriki semina pekee, kwa sababu kuna zoezi kubwa tutalifanya ambalo litakuwa msingi wetu kwa mwaka mzima. Wapo walioomba kupata nafasi hizi lakini hawataweza kushiriki semina, niwaambie kwamba haitawezekana. Kwa wasioshiriki wataweza kuendelea kunufaika na huduma ya PERSONAL COACHING, lakini hii ya watu 12, ni kwa wale watakaoshiriki semina.
  5. Hakutakuwa na njia nyingine yoyote ya kupata mafunzo ya semina hii tofauti na kuhudhuria. Hakutakuwa na rekodi yoyote ya sauti au video ya semina hii. Wapo walioomba sana turekodi na watakuwa tayari kulipia na kupata. Wapo niliowaahidi nitaangalia namna ya kufanya hilo, lakini halitawezekana. Hivyo kwa wale ambao hawataweza kuhudhuria semina ya mwaka huu, hakuna namna ya kupata mafunzo, mpaka tena semina ya mwaka kesho.
  6. Kutakuwa na mwongozo wa maisha ya mafanikio ambao tutaufanyia kazi kwa mwaka mzima, mwongozo huu unalenga yale maeneo muhimu sana kwenye maisha yetu ambayo yanajenga mafanikio yetu.
  7. Kupitia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, tutapata nafasi nzuri ya kukutana na kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu mafanikio kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, fanya malipo leo ili tuwe pamoja, tujifunze, tuhamasike na tuwe na mkakati wa kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

Nikukumbushe rafiki, mwisho wa kufanya malipo ni leo tarehe 31/10/2018, usipoteze nafasi hii ya kipekee inayokujia mara moja pekee kila mwaka.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; http://eepurl.com/dDZHvL