“I don’t think much of a man who is not wiser today than he was yesterday.” —Abraham Lincoln
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUWA BORA LEO KULIKO JANA…
Kama utaianza siku ya leo na kuimaliza, bila ya kujifunza kitu chochote kipya na bila ya kupiga hatua mpya, umechagua kuipoteza siku ya leo.
Kama jana ni afadhali ya leo, basi leo umeipoteza kabisa kwenye maisha yako.
Mafanikio kwenye maisha hayatokei kama ajali, huamki asubuhi na kujikuta umeshafika ulipotaka kufika.
Bali mafanikio yanafanyiwa kazi, kila siku kwa kupiga hatua ndogo ndogo na kuwa bora zaidi.
Mafanikio kwenye maisha ni mkusanyiko wa siku moja moja ambazo mtu ameishi vizuri na kwa mafanikio.
Kadhalika kushindwa ni mkusanyiko wa siku ambazo mtu amepoteza kwa kushindwa kuwa bora zaidi.
Ni rahisi kuichukulia siku moja kwa ukawaida sana, kuona haina madhara yoyote makubwa, lakini unachofanya siku moja, utakifanya tena siku nyingine na mwishowe inakuwa tabia ngumu sana kwako kuvunja.
Kazana kila siku kujijengea tabia nzuri, zinazokuwezesha wewe kufika kule unakotaka kufika.
Kazana kila siku mpya inayoanza ujifunze kitu kipya.
Usikubali siku yako iishi bila ya kuwa bora zaidi ya ilivyokuwa jana yako.
Ishi ndani ya siku yako, na iishi siku yako kama vile huna siku nyingine.
Fanya yale uliyopanga kufanya bila ya kuahirisha,
Jifunze vitu vipya,
Jaribu vitu vipya,
Na maisha yako yatakuwa ya mafanikio makubwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kuwa bora zaidi leo kuliko jana.
#Fanya#HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha