Mpendwa rafiki yangu,

Anayefurahia umasikini basi amechagua kuifanya dunia kuwa sehemu mbaya ya kuishi kwa kila mmoja wetu. Kila mmoja wetu anatakiwa auchukie umasikini, kila siku unatakiwa kuweka juhudi na kutangaza vita kabisa na umasikini na ikiwezekana upe kabisa talaka na usikuzoee katika maisha yako.

Wengi tunataka mafanikio huku tukiwa tumeweka mikono mifukoni, wengine wanaweka juhudi kubwa katika kubeti huku wakiamini kuwa iko siku watakuja kuwa na mafanikio. Hakuna mafanikio rahisi, kama umeshindwa kufanya kazi, basi umeamua kuwa rafiki wa umasikini katika maisha yako.

Watu wa japani wanasema siku ya kujua bahati yako ni pale utakapoamua kuchukua hatua. Nakubaliana na wajapani na mimi nakuambia hivi siku moja kubwa ya kuweka historia katika maisha yako ni pale utakapoamua kuchukua hatua dhidi ya ndoto yako.

Ni kweli najua una ndoto nyingi, je umeifanyia kazi ndoto yako? sasa unafikiri utafikia pale unapopataka kwa mdomo tu? Hapana kwa kuweka kazi, kila mmoja wetu anatakiwa kufanya kazi ili kuondokana na umasikini.

cropped-mimi-ni-mshindi

Watu wa benini nao hawajakosea kusema, dawa ya umasikini ni kazi. Hivyo nami nakazia hapo dawa ya umasikini ni kufanya kazi, kutoa thamani na mafanikio yatakuja yenyewe. Mafanikio ni magumu kupatikana hivyo nayo yanachagua kwenda kwa mtu aliye na nidhamu hivyo wewe kama huna nidhamu ya maisha usitegemee mafanikio yatakufuata hapo ulipo.

SOMA; Hawa Ndiyo Watu Wanaopendelewa Na Historia

Fanya kazi, chukua hatua mwaka ndiyo huo unaisha, kila siku unaweka mipango ya kufanya lakini hufanyi. Hebu leo chukua hatua, angalau ujivunie kabla ya mwaka huu kuisha ulifanikiwa kuchukua hatua hii. Usiangalie matokeo utakayoyapata bali, angalia umechukua hatua, wengi wanahofu matokeo hivyo wanaogopa kuchukua hatua.

Hatua ya kuchukua leo,jenga historia leo kwa kuchukua hatua sahihi. Miaka ijayo utajikumbuka sana kwa maamuzi na hatua ulizochukua leo.

Kwahiyo, andaa maisha yak oleo, usikubali kuja kuteseka hapo baadaye wakati sasa una nguvu. Tumia nguvu zako vizuri sasa ili baadaye uwe na maisha mazuri.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana!