Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa nakuambia hakuna kipindi kibaya cha kuweka malengo na mipango kama kipindi cha mwaka mpya.

Kwa sababu hichi ni kipindi ambacho watu wanasukumwa na hisia na kuweka malengo na mipango mikubwa, lakini haichukui muda wanaachana na malengo na mipango hiyo.

Watu wengi huwa wanapelekwa na upepo wa MWAKA MPYA MAMBO MAPYA, wanajiwekea mipango mikubwa kwa mwaka huo husika, na hata baadhi ya hatua wanaanza kuchukua. Lakini mpaka mwezi wa kwanza unapoisha, wengi wanakuwa wameshaachana na malengo na mipango yao.

Kila mwanzo wa mwaka watu wanakuwa na mipango na wanaanza kuchukua hatua. Tembelea maeneo ya mazoezi mwanzo wa mwaka na utakuta watu wengi wanafanya mazoezi. Watu wengi wanaanza biashara zao mwanzo wa mwaka. Wengi pia wanaanza ujenzi na shughuli nyingine mwanzo wa mwaka. Na pia mwanzo wa mwaka watu huwa wanajituma sana kwenye kazi zao.

2018-2019

Lakini mwezi januari unapoisha, wengi wanakuwa wameshaachana na ule upya wa mwaka, mpaka unapofika mwezi machi, asilimia 99 ya wale waliokuwa na mipango mikubwa wanakuwa wameshaachana nayo kabisa na wanarudi kwenye maisha yao ya mazoea.

Wanasubiri tena mpaka mwaka mpya mwingine ufike na mzunguko huo unajirudia tena. Watu wengi wamekuwa wanafanya hivi maisha yao yote. Tafiti zilizofanywa nchini marekani zinaonesha mtu mmoja huweka malengo yale yale na bila kuyafikia kwa zaidi ya miaka 10. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani tatizo hili lilivyo kubwa.

Katika kuondokana na kikwazo hichi, na kwa sababu jukumu langu kubwa ni kukuandalia wewe maarifa ya kukuwezesha kupiga hatua zaidi, nilikushirikisha jinsi ya kuishi bila ya malengo, yaani unauanza mwaka siyo kwa kuandika yale malengo uliyozoea kuandika kila mwaka, bali unaandika ndoto kubwa na maono uliyonayo kwa mwaka huo. Badala ya kujipa malengo ambayo huyatekelezi, nilikushirikisha njia ya kutembea na picha kwenye akili yako, ambayo haitakutoka mara zote.

SOMA; Tumia Nafasi Ya Leo Kufanya Maamuzi Haya Muhimu Kwa Mafanikio Yako Makubwa.

Njia hii ni bora sana na ina matokeo mazuri sana maana inazipa akili zetu kazi kubwa ya kututengenezea mazingira yoyote tunayoyataka. Lakini njia hii haikueleweka vizuri na wengi, nafikiri ni kwa sababu tumeshazoea sana malengo.

Hivyo nilikuja na njia ya pili, ambayo inatumia malengo pamoja na taswira ya ndoto na maono ambayo mtu unayo. Lakini njia hii ya pili inakuepusha na ule mhemko wa kuweka malengo kipindi cha mwaka mpya, kipindi ambacho wengi wanasukumwa na hisia ya kundi.

Njia hii ni kuanza mwaka mpya mapema kabisa kabla watu wengine hata hawajafikiria kuuanza. Hii inakupa nafasi ya kutafakari kwa kina vitu gani ni muhimu kwa maisha yako na jinsi gani ya kuvifikia, badala ya kusukumwa na mipango ya wengine.

Hivyo rafiki, kila tarehe moja ya mwezi wa kumi na moja kila mwaka, nimekuwa nawashirikisha watu kama siku ya kuuanza mwaka mpya wa mafanikio. Unapouanza mwaka wa mafanikio mapema zaidi, inakuwa rahisi kwako kutafakari yale muhimu, kuweka mipango ambayo ni sahihi kwako na kuanza kuchukua hatua mapema.

Pale mwaka mpya unapofika, na watu wanakimbizana kuweka malengo na mipango, wewe unakuwa mbele zaidi kwa siku 60, na kama hujajua rafiki, siku 60 ndiyo siku ambazo tafiti zinaonesha zinahitajika kwa mtu kujenga tabia mpya kwake.

Hivyo wakati wengine wanakimbizana na mihemko ya mwaka mpya, wewe unakuwa tayari umeshauweka mwaka wako vizuri na unachukua hatua kubwa kabisa.

Hivyo rafiki yangu, nikupongeze na kukukaribisha kwenye MWAKA MPYA WA MAFANIKIO 2018/2019 ambao unaanza tarehe 01/11/2018 na kumalizika tarehe 31/10/2018.

Tumia siku hii ya leo kutafakari kwa kina nini unataka kwenye maisha yako kwa miezi 12 ijayo, wiki 52 zijazo na siku 365 zijazo. Jijengee taswira ya maono yako makubwa uliyonayo, ya muda mrefu na muda mfupi, kisha ona kwa mwaka mmoja unaokuja ni hatua kiasi gani utakuwa umepiga.

Panga hatua kubwa utakazochukua kila siku yako ili kuweza kufikia malengo na mipango uliyojiwekea. Na muhimu zaidi, andika kabisa kwenye kijitabu chako, nini unataka na hatua zipi utakazochukua kila siku.

Kwa wale watakaohudhuria SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 itakayofanyika jumamosi hii ya tarehe 03/11/2018 tutafanya zoezi hili kwa pamoja. Tutaweka mipango ya mwaka huu mpya wa mafanikio 2018/2019 na kupanga hatua kubwa ambazo tunakwenda kuchukua kwa mwaka mzima ili kuweza kufanikiwa zaidi.

Kwa wale ambao hawajapata nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, ipo nafasi ya kuishi mwaka mpya wa mafanikio kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, kila siku utajifunza na kuweza kuchukua hatua ili kufanikiwa zaidi.

Nakukaribisha sana kwenye semina kwa wale waliopata nafasi, na kwa wengine nawakaribisha sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ambapo kuna nafasi chache, tusafiri kwa pamoja kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuweza kupiga hatua zaidi.

Rafiki, mwaka mmoja ukiuangalia kwa mbele utaona ni mrefu sana, lakini ukiuangalia kwa nyuma, unaona ni mfupi mno. Yaani mwaka unapoanza utaona una siku nyingi mbele yako, lakini unapoisha unaona siku zilikuwa chache.

Nimejitoa kuhakikisha wewe unafanikiwa sana, kwa sababu najua wewe ukifanikiwa na mimi ndiyo nafanikiwa. Hivyo kama umejitoa kweli kwa ajili ya mafanikio, basi karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tuwe pamoja.

Rafiki, nimalize kwa kukuambia kwamba, ukiuanza mwaka mpya wa mafanikio leo, utakuwa mbele kabia ya wengine na utajitenga na kundi kubwa la wale wanaofanya kwa mazoea na kufuata kundi. Na hatua ya kwanza kabisa ya kufanikiwa kwenye maisha, ni kuweza kuachana na kundi.

Nakutakia kila la kheri kwenye MWAKA MPYA WA MAFANIKIO 2018/2019, upangilie vizuri na chukua hatua kila siku kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora zaidi. Karibu pia tuwe pamoja kwenye safari hii kupitia KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 ili kupata maelekezo zaidi.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)

Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha

Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu

Usomaji