Ni kwamba wanahamishia chuki yao kwa wengine pia.
Watu wanaojichukia wenyewe, huwa wanatafuta kitu cha kuchukia kwa wengine pia, hata kama ni kitu ambacho hakina tatizo lolote.
Mtu anayejichukia mwenyewe, hawezi kufanya kazi zake vizuri na hivyo hawezi kufanikiwa. Sasa anapoona wengine wamefanikiwa, anawachukia kwa sababu wao wamepiga hatua kuliko yeye. Hakuna tatizo lolote kwa mtu kufanikiwa, lakini wenye chuki hawawezi kuliona hilo.
Watu wanaojichukia wao wenyewe wanajaza chuki kwenye dunia, wanaambukiza chuki na tunapaswa kuwajua na kuwaepuka.
Hawa ni watu ambao kwa kitu kidogo wanajibu kwa namba ambayo haiendani na kitu husika. Ni watu ambao wakiona wengine wanapiga hatua kwenye maisha yao, wanachukia na kuona labda kwa wengine kupiga hatua kunawarudisha wao nyuma.
Watu wenye chuki wanaididimiza dunia.
Watu wenye upendo wanainyanyua dunia, wanaifanya dunia kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi.
Hivyo dunia inachotaka ni watu wengi zaidi wenye upendo kuliko wenye chuki.
Kuwa na upendo na sambaza upendo, ndiyo kitu pekee kitakachoiinua dunia, ndiyo kitu muhimu wewe na dunia nzima inahitaji ili kuwa bora zaidi.
Tatizo la watu wenye chuki kama tulivyoona, siyo tu chuki zinakaa ndani yao, bali wanazisambaza na kwa wengine pia na kuididimiza dunia.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,