Siku mpya,
Siku bora,
Na siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA UNATAKA MAJI, CHIMBA SHIMO MOJA NA ZAMA CHINI ZAIDI…
Kama unachimba kisima ili upate maji, hutayapata kwa kuchimba mashimo mengi mafupi mafupi.
Badala yake unahitaji kuchimba shimo moja kisha kuzama chini zaidi.
Unahitaji kwenda kwenye kina kirefu zaidi na huko ndipo utakapokutana na maji safi na ya kudumu.
Kuchimba mashimo mengi mafupi mafupi kunakupotezea muda, kunakucheleweaha na kunapoteza nguvu zako.
Kushimba shimo na kuwa na upana mkubwa pia bado hakutakupatia maji.
Unahitaji kuzama chini, kwenda kwenye kina kirefu zaidi.
Kama unataka kufanikiwa kwenye maisha, chagua kitu kimoja, au vichache kisha zama chini zaidi, zama kwenye vitu hivyo kwa kwenda ndani zaidi, kuweka juhudi zaidi na kubobea zaidi.
Kuhangaika na vitu vingi kwa wakati mfupi hakutakupatia mafanikio unayotaka.
Kukazana na vitu vingi, hata kama unavipenda kiasi gani, kunatawanya nguvu zako na hazitaweza kukusaidia.
Chimba shimo moja, na zama chini, nenda kwenye kina kirefu mpaka ufike kwenye mwamba wenye maji matamu na yasiyokauka, hayo ndiyo mafanikio halisi na yasiyokuwa na ukomo.
Uwe na siku bora sana rafiki, siku ya kuchagua yale machache muhimu sana ya kufanya, kisha zama chini zaidi, nenda ndani zaidi, bobea zaidi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha