“Clean your room before you save the world.”
Ni siku nyingine mpya kwetu,
Siku bora na ya kipekee sana,
Siku ambayo tuna nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Hii ndiyo ile siku ambayo jana tulisema kesho tutafanya.
Ni rahisi sana na leo kusema kesho nitafanya, lakini hutafanya.
Hivyo kama kuna kitu muhimu, kifanye leo hii na usikipeleke kesho.
Tunaiendea siku hii kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tutafanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari SAFISHA CHUMBA CHAKO KABLA HUJAIOKOA DUNIA…
Kila mmoja wetu huwa anakuwa na mipango mikubwa sana kwenye maisha yake.
Mipango ya kufanya makubwa sana ambayo yatainufaisha sana dunia.
Lakini mipango hii huwa inabaki kuwa mipango na hakuna hatua kubwa ambazo mtu anachukua.
Wengi wanapokuwa na mipango hiyo mikubwa, wanashindwa kujua waanzie wapi, hivyo wanabaki wakipanga na kupangua kila wakati.
Njia pekee ya kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yako, ni kwa kuanza kuchukua hatua ndogo ndogo ambazo zipo ndani ya uwezo wa kila mmoja wetu.
Anza kusafisha chumba chako kabla hujaiokoa dunia, hakuna anayeshindwa kusafisha chumba chake.
Kwa kuanza na hatua ndogo kama hizi, unaweza kupiga hatua kubwa zaidi kwenye maisha yako.
Kwa kila hatua ndogo unayopiga, unaziona fursa za kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
Ni vizuri sana kuwa na malengo na mipango mikubwa, lakini kama huchukui hatua unajidanganya wewe mwenyewe.
Ni bora kuchukua hatua, hata kama ni ndogo kiasi gani, kuliko kutokuchukua hatua kabisa.
Ukisafisha chumba chako, unaziona fursa zaidi za kuyasafisha maisha yako na baadaye unajikuta umeiokoa dunia.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchukua hatua ndogo kwenye kila mipango mikubwa uliyonayo kwenye maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha