“Happiness is neither virtue nor pleasure nor this thing nor that, but simply growth. We are happy when we are growing.” — William Butler Yeats

Ni siku nyingine nzuri sana kwetu,
Siku ya mafanikio makubwa kwetu.
Tumeipata nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FURAHA NA UKUAJI…
Furaha ni pale unapokua zaidi, unapopiga hatua kutoka chini na kwenda juu zaidi.
Kadiri unavyokua, ndivyo unavyokuwa na furaha zaidi, inayokuletea hamasa zaidi ya kukuwezesha kukua zaidi.

Sheria ya asili ni kukua, kuongezeka, kupiga hatua zaidi.
Ndiyo maana kila utakachoangalia kwenye asili, kinakua na kuongezeka zaidi.
Hata mti uwe mkubwa kiasi gani, bado utaendelea kukua na kuzakisha miti mingine mingi zaidi.
Shamba likiwa halijapandwa kitu, yataota majani na magumu, ni sheria ya asili kukua.

Hivyo hata kwetu binadamu, ukuaji na kupiga hatua zaidi ni sheria ya asili.
Na kadiri tunavyokua na kupiga hatua zaidi, ndivyo tunavyokuwa na furaha na maisha yetu kuwa bora zaidi.
Na hili ndiyo linawasumbua wale wanaofikiri kwamba wakishafika hatua fulani ya mafanikio hawahitaji kufanya tena chochote. Wakifika hatua hiyo na kuacha kufanya walichokuwa wanafanya, maisha yanakuwa ya hovyo zaidi kwao na kukosa furaha licha ya kuwa na mafanikio makubwa.

Rafiki, jikumbushe hili kila siku, kwamba furaha ipo kwenye ukuaji, hivyo kila siku unapaswa kukua zaidi.
Leo unapaswa kuwa bora kuliko ulivyokuwa jana.
Kama leo ni sawa na jana, basi leo umeipoteza, leo hujakua, na hilo litakupelekea usiwe na furaha.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukua zaidi ili kutengeneza furaha zaidi kwenye maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha