“There’s no right way to do the wrong thing and there’s no wrong way to do the right thing.”
Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni siku ambayo tumepata nafasi ya kipekee kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Siyo wote ambao wameipata siku hii wakiwa wazima wa afya na wenye nguvu ya kwenda kupambana.
Hivyo ni upendeleo wa kipekee sana kwetu kuipata siku hii tukiwa vizuri.
Tusipoteze nafasi hii, bali tuitumie vyema sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KITU SAHIHI NA NJIA SAHIHI.
Rafiki, mara zote unapaswa kufanya kile ambacho ni sahihi kwako, na ukiweza kulisimamia hili siku zote, utaweza kufanya makubwa sana.
Watu wengi wamekuwa wanafanya kila kinachojitokeza mbele yao, hata kama siyo sahihi.
Hili linawapotezea muda na hata nguvu ambazo kama wangetumia kwa yaliyo sahihi, wangepiga hatua zaidi.
Hakuna njia sahihi ya kufanya kitu ambacho siyo sahihi. Hivyo kama kitu siyo sahihi, hata ukifanye kwa njia gani, bado kitabaki kuwa siyo sahihi.
Pia hakuna njia isiyo sahihi ya kufanya kikicho sahihi.
Kama kitu ni sahihi, kukifanya kwa namna yoyote ni sahihi.
Hivyo swali lako la kwanza kujiuliza kabla ya kufanya chochote ni je, kitu hiki ni sahihi au siyo sahihi?
Kama siyo sahihi, wala usiendelee kujidanganya,
Usijiambie mbona kila mtu anafanya,
Usijiambie unafanya mara moja tu,
Usijiambia haina ubaya sana.
Kama kitu siyo sahihim kitabaki kuwa siyo sahihi hata kama utajiteteaje.
Na wewe utakuwa mtu wa kwanza kujihukumu mwenyewe, kwa sababu unajua umefanya kisicho sahihi.
Ukawe na siku bora sana leo mwanamafanikio, siku ya kifanya yale yaliyo sahihi pekee.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha