“The more value you deliver in life, the most freedom and power you have.”

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari THAMANI = UHURU.
Kiwango cha uhuru ulichonacho kwenye maisha yako, inategemea na kiwango cha thamani unayotoa.
Kama unayoa thamani kubwa, unakuwa na uhuru mkubwa.
Kama unatoa thamani ndogo, uhuru wako unakuwa mdogo pia.

Hivyo kama unataka uhuru zaidi kwenye maisha yako, kama unataka kuwa na nguvu na mamlaka zaidi, toa thamani kubwa zaidi.
Wale wanaotoa thamani kubwa ndiyo wanaotafutwa na kutegemewa zaidi.
Wale wanaotoa thamani kubwa ndiyo wanaolipwa zaidi.
Na wale wanaotoa thamani kubwa ndiyo wenye nguvu ya kutaka kupata zaidi.

Kama unachofanya ni cha kawaida, kile ambacho kila mtu anaweza kufanya, huna uhuru wa kuamua ufanyeje, na wala huna nguvu ya kutaka ulipwe zaidi. Kwa sababu hata ukiacha kufanya, wapo wengine wengi ambao wapo tayari kufanya.
Ila pale unapofanya kitu cha tofauti na pekee, kitu ambacho hakuna wengine wanaoweza kufanya, unakuwa huru kuchagua ufanyeje na una nguvu ya kuamua ulipweje.
Uzuri ni kwamba, ndani ya kila mmoja wetu, upo uwezo mkubwa wa kutoa thamani zaidi.
Kazi yetu ni kujua na kutumia uwezo huo mkubwa.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kutoa thamani kubwa zaidi ili uwe huru kwenye ufanyaji na uwe na nguvu ya kufanya maamuzi ya unalipwaje.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha