“Be pleasant until ten o’clock in the morning, and the rest of the day will take care of itself.” — Elbert Hubbard
Ni siku nyingine mpya kwetu rafiki.
Siku ambayo tumepata nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari IMILIKI SIKU YAKO…
Wahenga walisema; nyota njema huonekana asubuhi
Na wakaenda mbali zaidi na kusema; biashara ni asubuhi, jioni mahesabu
Kuna nguvu kubwa sana kwenye asubuhi yako.
Hivyo kama unataka kuimiliki siku yako, imiliki asubuhi yako.
Na kama Elbert Hubbard anavyotuambia, ukiwa mtulivu mpaka saa nne ya asubuhi, siku nzima itakwenda vizuri sana kwako.
Asubuhi ndiyo muda bora sana kwako kuitengeneza siku yako kuwa ya ufanisi mkubwa.
Asubuhi ndiyo wakati ambao una nguvu kubwa kiakili na kimwili, wakati mzuri kwako kufanyia kazi yale makubwa, magumu na ya muhimu.
Ukiweza kuidhibiti asubuhi yako, ukiweza kufanya yale uliyopanga kufanya, yale ambayo ni muhimu zaidi, utaweza kuikiliki siku yako na maisha yako pia.
Na unachohitaji ni kuwa mtulivu tu mpaka kufika saa nne asubuhi.
Hii ina maana usifanye kitu chochote cha hivyo tangu unapoamka mapema mpaka kufika saa nne asubuhi.
Hii ina maana usipoteze hata dakika moja katika muda huo.
Inamaanisha hakuna kelele, hakuna habari, hakuna mitandao ya kijamii.
Fikiria kama uneamka saa 10 asubuhi, na ukadhibiti muda wako mpaka saa 4 asubuhi, utakuwa umepata masaa 6 yenye ufanisi mkubwa sana.
Kwa ndani ya muda huo, utajikuta umefanya makubwa kuliko mtu wa kawaida anavyofanya jwa siku tatu.
Na hapo siku ndiyo kwanza inaanza, una mida mwingine mwingi mbele yako.
Kuimiliki siku yako, kuweza kufanya makubwa na maisha yako, miliki asubuhi yako, kuwa mtulivu mpaka kufika saa nne, na siku itakwenda vizuri sana kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa mtulivu na kutokufanya chochote cha hovyo mpaka kufika saa nne asubuhi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha