Rafiki yangu mpendwa, ipo kauli ambayo watu wengi huwa wanapenda kuitumia linapokuja swala la fedha.

Kauli hiyo ni kwamba watu wote hatuwezi kuwa matajiri, kwamba hata iweje, bado kutakuwa na watu ambao ni masikini na wengine matajiri.

Pia imewahi kusemwa sana kwamba ukichukua fedha za watu wote, kisha ukawagawia watu wote kiasi sawa, baada ya muda bado utakuta wachache ni matajiri na wengi ni masikini.

Watu wamekuwa wakitafuta nini kinawafanya wachache kuwa matajiri na wengi kuwa masikini.

Ukiangalia eneo, ndani ya eneo moja unakuta kuna matajiri na masikini.

Ukiangalia kazi au aina ya biashara, kwenye kila kazi au biashara kuna ambao wana utajiri na kuna ambao ni masikini.

Na hata ukiangalia ndani ya familia, watoto waliozaliwa na baba na mama mmoja, kuna ambao wanakuwa matajiri na wengine kuwa masikini.

Ni rahisi kusema kwamba wanaotajirika wana bahati, kwa sababu hakuna kinachowatofautisha sana na wale wanaobaki kwenye umasikini.

FEDHA KWA BLOG

Lakini baada ya tafiti za muda mrefu, siri imefichuka, na siri kuu ipo kwenye tabia za kila siku. Zile tabia ndogo ndogo tunazofanya kila siku, ndiyo zinazochangia kwenye utajiri au umasikini.

Hivyo kama unataka kutengeneza utajiri mkubwa kwenye maisha yako, kazi yako ipo kwenye siku moja tu.

Jinsi unavyoiishi siku yako moja ndiyo unavyoziishi siku zako nyingine na hilo linakupeleka kwenye mafanikio au kushindwa.

Kwa kuwa nakupenda sana wewe rafiki yangu, na kwa kuwa wajibu niliojipa ni kukupa wewe maarifa sahihi ili uweze kufanya maamuzi bora na kuchukua hatua za kuyafanya maisha yako kuwa bora, nimekuandalia semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Hii ni semina ambayo utajifunza tabia kumi za kuishi kwenye kila siku yako, ambazo zitakuwezesha kufika kwenye utajiri na mafanikio makubwa.

Semina hii siyo ya kujifunza na kufurahi, badala yake ni semina ya kutengeneza msingi mpya wa mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Na kama kuna maamuzi bora ambayo utakuwa umeyafanya kwenye maisha yako yote hapa dunia, basi yatakuwa ya kushiriki semina hii na kuanza kuishi maisha yako kwa msingi utakaojifunza.

Semina itaendeshwa kwa mtandao wa wasap, hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote duniani, huhitaji kusafiri wala kuacha chochote unachofanya sasa. Ni wewe kutenga muda wa kufuatilia masomo kila siku na kupanga kuchukua hatua.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/01/2019. Kila siku kwa siku kumi utajifunza tabia moja muhimu ya kuishi kwenye kila siku yako ili kufikia utajiri mkubwa kwenye maisha yako.

Ili kushiriki semina hii unapaswa kulipa ada ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=), lakini kama wewe tayari ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA huhitaji kulipa ada ya kushiriki semina hii. Wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA wanashiriki semina hii moja kwa moja kama sehemu ya uanachama wao.

Mwisho wa kulipa ada ya kushiriki semina hii ni tarehe 02/01/2019, baada ya tarehe hii hutaweza kupata tena nafasi.

Namba za kufanya malipo ya semina ni 0755 953 887 au 0717 396 253 majina ya namba hizo ni Amani Makirita.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap namba 0717396253 wenye majina yako kamili na kwamba umelipia semina, na hapo utawekwa kwenye kundi maalumu la semina.

Pia unaweza kujiunga na kundi la semina na ukaendelea kupata taarifa zaidi kuhusu semina. Kujiunga na kundi la semina hii tumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv  (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).

Karibu sana rafiki yangu kwenye semina hii ya kipekee sana kwako kuweza kujijengea msingi imara wa mafanikio makubwa.

Nimekuandalia maarifa bora kabisa ambayo hupaswi kuyakosa kama upo makini na maisha yako. Chukua hatua sasa ya kujiunga na SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI na uweze kujijengea msingi wa mafanikio makubwa.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge