“How many have laid waste to your life when you weren’t aware of what you were losing, how much was wasted in pointless grief, foolish joy, greedy desire, and social amusements—how little of your own was left to you. You will realize you are dying before your time!” —SENECA, ON THE BREVITY OF LIFE, 3.3b

Ni siku nyingine mpya na nzuri sana kwetu rafiki,
Ni nafasi nzuri tuliyokuwa tunaisubiri ili kuweza kufanya yale ambayo ni bora na ya kipekee.
Kwa kulala mapema na kuamka mapema, tunaweza kupata zawadi kuu tatu ambazo ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA.
Na kwa msingi wetu wa maisha ya mafanikio ambao ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tunaweza kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIWE NA HURUMA KWW VITU VISIVYOKUWA NA UMUHIMU…
Japokuwa maisha ni mafupi na muda wetu ni mdogo, bado pia tumekuwa tunapoteza muda, maisha na nguvu zetu kwenye mambo ambayo hayana umuhimu wowote kwetu.
Mambo ambayo tunaweza kusema ni ya kijinga na hayatuongezei chochote.
Mambo kama hasira, wivu, kufuatilia maisha ya wengine na hata kufikiria wengine watakuchukuliaje kwa kile unachofanya, hayana manufaa yoyote kwako zaidi ya kupoteza muda wako, nguvu zako na hata maisha yako.
Kwa sababu rasilimali maisha unazoweka kwenye mambo hayom huwezi kuziweka kwenye mambo mengine bora kwako.

Njia pekee ya kuondokana na mambo haya yanayokupotezea muda ni kutokuyaonea huruma, kuwa katili kabisa na kusema HAPANA.
Sema hapana kwenye kila jambo ambalo halichangii wewe kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
Sema hapana kwa kila jambo ambalo halihusiani na aina ya maisha unayoyataka.
Hata kama kila mtu anafanya, kama siyo sahihi kwako usifanye.

Jua yale ambayo ni muhimu kwako na yale kipaumbele hayo, kazi na biashara zako, afya yako, kujifunza zaidi, kipato chako, mahusiano yako. Hivi vinapaswa kupata muda na nguvu zaidi ili uweze kuoiga hatua zaidi.
Na muda na nguvu unazohitaji kuweka kwenye maeneo hayo muhimu, unapaswa kuzitoa kwenye yale maeneo ambayo siyo muhimu.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kusema HAPANA kwa yale yote ambayo siyo muhimu kwako, hata kama umeshayafanya kwa muda mrefu. Unaweza kuanza leo na ukatengeneza matokeo makubwa na ya tofauti kwenye maisha yako.
#SemaHapana, #KuwaNaVipaumbele, #TunzaMudaNaNguvuZako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha