Rafiki yangu mpendwa,

Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa nimekuwa nakupa taarifa za semina ya kuuanza mwaka 2019.

Semina hiyo inakwenda kwa jina la TABIA ZA KITAJIRI.

Ndani ya semina hii tunakwenda kujifunza tabia kumi za kuishi kila siku ambazo ukizielewa na kuzifanyia kazi basi utaweza kutengeneza utajiri na mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote duniani, huhitaji kusafiri wala kuacha shughuli zako. Unachohitaji ni kutenga muda kila siku wa kufuatilia mafunzo haya na kuchukua hatua.

FEDHA KWA BLOG

Semina inaanza kesho tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/10/2019.

Zitakuwa ni siku 10 za kujifunza, kuhamasika na kuanza kuchukua hatua zitakayoyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Mwisho wa kupata nafasi ya kujiunga na semina hii ni leo tarehe 02/01/2019, saa 12 jioni. Baada ya muda huu kupita nafasi za kujiunga na semina hii zitafungwa ili maandalizi ya semina yaweze kuanza na watu kujifunza.

Kama unataka kuuanza mwaka 2019 kwa utofauti na upekee mkubwa, basi nafasi ndiyo hii.

Ili kushiriki semina hii unapaswa kulipa ada ya kushiriki semina ambayo ni tsh 20,000/= (elfu 20). Malipo yanafanyika kupitia namba 0755 953 887 au 0717 396 253, majina ya namba hizi ni AMANI MAKIRITA.

Kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii, tuma malipo yako sasa hivi na ukishatuma fedha tuma ujumbe kwa njia ya wasap namba 0717396253, ujumbe uwe na majina yako kamili.

Mimi kama rafiki yako ninayekupenda na kukujali sana, ambaye kila siku nimekuwa nakushirikisha maarifa mengi na bora sana bure kabisa, nakuambia usikose semina hii. Ada unayolipa ni uwekezaji mdogo ambao utaleta matokeo makubwa sana kwenye maisha yako.

Tabia ndiyo msingi wa maisha, uko hapo ulipo sasa kutokana na tabia ulizojijengea huko nyuma, iwe kwa kujua au kwa kutokujua. Na ili kupiga hatua zaidi, lazima ujijengee tabia bora zaidi. Semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI itakuwezesha kujijengea na kuishi tabia bora kabisa kila siku.

Rafiki, kama huna kabisa fedha ya kushiriki semina hii basi omba, changisha au uza chochote ambacho hakikuzalishii kwa sasa, ili uweze kuwekeza fedha hiyo kwenye elimu itakayokusaidia kwa maisha yako yote.

Na kama una wasiwasi kwamba hakuna kipya utakachojifunza, nakupa nafasi ya bure kabisa ya kushiriki semina hii. Unachofanya ni kulipia ada ya kushiriki semina hii, kufuatilia masomo haya kwa kina, na mwisho wa semina kama utaona hakuna jipya na la maana ulilojifunza basi unaniambia na ninakurudishia ada uliyolipa.

Kila semina na mafunzo ninayoandaa nahakikisha kila mtu anaondoka na vitu vya kufanyia kazi, ambavyo vitayafanya maisha yake kuwa bora zaidi. Na kwenye semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI, nakwenda kukupa kanuni kuu ya maisha, ambayo ukiishi kila siku, maisha yako yatakuwa bora zaidi.

MUHIMU ZAIDI; Kama unataka kushiriki semina na hutumii mtandao wa wasap, nakupa nafasi ya kupokea mafunzo ya semina hii kwa njia ya email. Hivyo lipia ada ya kushiriki semina hii na nitumie ujumbe wa simu wa kawaida kwamba umelipia semina na utashiriki kwa njia ya email na unipe email yako.

MUHIMU PIA; Kama una ndugu, jamaa au rafiki wa karibu ambaye unapenda kumsaidia na maisha yake yawe bora, basi mlipie ashiriki semina hii. Tuma ada kwa ajili yake na nitumie majina yake pamoja na wewe kumwarifu kuhusu semina kisha atapata nafasi ya kushiriki semina hii bora sana kwa kila mmoja wetu.

Karibu sana sana rafiki yangu, usikose kabisa nafasi hii ya kipekee sana kwako kuuanza mwaka 2019 kwa mafanikio makubwa.

Lipia sasa hivi tsh 20,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kwa wasap namba 0717396253. Ni rahisi kama hivyo na kuanzia kesho utaanza kujijenga msingi wa mafanikio yako makubwa.

Rafiki, neno langu kwako ni moja, usikose nafasi hii.

Karibu sana rafiki yangu.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge