Kama unaacha kufanya kitu muhimu kwako kwa sababu hutaki watu wakuchukie, unajichelewesha kufanikiwa.

Chuki ni kazi ya watu, na watu watakuchukia kwa sababu ambazo hazipo ndani ya uwezo wako.

Wapo watu ambao watachagua kukuchukia kwa sababu tu umechagua kuishi maisha yako, na hakuna chochote utakachofanya ukaondoa chuki waliyonayo juu yako.

Usiache kufanya kitu muhimu kwako kwa sababu hutaki watu wakuchukie, watu watakuchukia na hiyo siyo juu yako.

Watu watachagua kukuchukia kwa namna wanavyoamua wenyewe, huwezi kubadili hilo.

Na wale watu ambao ni wa karibu zaidi kwako ndiyo watakaoongoza kwa kuwa na chuki juu yako. Watakuchukia, watakuangusha, au hata kuamua kukuumiza.

Hali hii inaweza kukuvuruga sana, usielewe kwa nini watu uliowategemea wawe upande wako wanakuwa wapinzani wako.

Elewa kwamba unapochagua kufanya vitu bora, unapoamua kuachana na mazoea, utaibua chuki ndani ya wengine na huna namna ya kuondoa hilo.

Jukumu kubwa kwako ni kuishi maisha yako, kufanya yale ambayo ni muhimu kwako na kuwaacha wengine wachague kufanya yale waliyochagua.

Usipoteze muda wako kujiuliza kwa nini watu wanakuwa na chuki kwako kwa kuchagua kuishi maisha yako, hutapata jibu na hata ukilipata hutakuwa na cha kufanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha