“Don’t return to philosophy as a task-master, but as patients seek out relief in a treatment of sore eyes, or a dressing for a burn, or from an ointment. Regarding it this way, you’ll obey reason without putting it on display and rest easy in its care.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.9

Tunayo siku nyingine mpya na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari; FALSAFA KAMA DAWA YA ROHO…
Usiiendee falsafa kama jukumu la kutekeleza,
Bali iendee kama mgonjwa anayetafuta matibabu ya ugonjwa alionao.
Unapokuwa mgonjwa unahangaika mpaka upate matibabu, na hata kama matibabu yanaumiza, utayavumilia kwa kuwa unajua yana manufaa kwako.

Hivi ndivyo tunavyopaswa kuichukulia falsafa, hasa falsafa ya Ustoa.
Kuiendea kama matibabu ya roho zetu, kwa sababu inatuwezesha kujali yale ambayo ni muhimu na kuachana na yasiyokuwa muhimu.

Tunaishi kwenye dunia yenye mambo mengi na kelele za kila aina, dunia ambayo ni rahisi sana kusahau kusudi letu la ndani na kusahau uwezo mkubwa tulionao tukishajichanganya kwenye kelele hizi.
Ndiyo maana mara kwa mara tunapaswa kuachana na kelele hizo na kurudi kwenye falsafa.
Kuna wakati itatubidi kuacha kile tulichozoea na kurudi kwenye utulivu wetu wa ndani, ili kuweza kuona vizuri kile tunachotaka.

Turudi kwenye falsafs ya ustoa kila mara kwa kuwa ndiyo mwongozo wetu mkuu wa maisha ya utulivu, yenye furaha na mafanikio makubwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuirudia falsafa ya Ustoa kama matibabu ya roho yako.
#FalsafaTibaYaRoho, #UstoaNguzoYaMaisha, #UtulivuHitajiLaMaishaBora

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha