“Many are harmed by fear itself, and many may have come to their fate while dreading fate.”
—SENECA, OEDIPUS, 992
Tumeipata nafasi nyingine nzuri sana kwetu mwanamafanikio.
Ni fursa ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari; HOFU NI MAUMIVU YA KUJITAKIA…
Mara nyingi tumekuwa tunahofia vitu ambavyo hata havitokei,
Tunaumia kwa hofu ya vitu kuliko hata tunavyoumia kwa vitu hivyo.
Tunajisumbua na vitu ambavyo hata bado havijatokea, na hata uwezekano wake wa kutokea ni mdogo mno.
Hofu ni maumivu ya kujitakia na ambayo hayana manufaa kwa sababu hata kama utahofia kwa kiasi gani leo kuhusu kesho, hakuna lolote unaloweza kubadili kuhusu kesho.
Unapohofia leo kitu ambacho kinaweza kutokea kesho au siku zijazo, unakuwa umechagua kuipoteza leo, lakini pia unakuwa hujabadilo chochote kwa kesho yako.
Amua leo kuondokana na maumivu hayo ya kujitakia, usikubali hofu ya chochote ikutawale.
Chagua kuishi leo, chagua kufanya kile kilicho mbele yako, na chochote kinachokupa hofu jiambie utakikuta na utakikabili.
Na mara nyingi sana, unachohofia huwa hata hakitokei.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutoruhusu hofu yoyote ikuumize, siku ya kuchagua kuishi leo kwa kufanya kilichopo mbele yako.
#HofuMaumivuYaKujitakia, #IshiLeo, #UnayohofiaHayatokei
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha