Pale unapokuwa njia panda katika kufanya maamuzi, ipo sheria inayoweza kukurahisishia zoezi la kufanya maamuzi yako.

Sheria hiyo ni ya kumi tatu, ambapo unajiuliza maswali matatu yenye kumi ndani yako na yatakuwezesha kujua kipi sahihi kufanya.

Swali la kwanza ni je kitu hiki kitakuwa muhimu kwangu dakika kumi zijazo? Hapa unajiuliza kama dakika kumi zijazo kile ambacho uko njia panda nacho kitakuwa muhimu kwako.

Swali la pili ni je kitu hiki kitakuwa muhimu kwangu miezi kumi ijayo? Kama kwa miezi kumi inayokuja kitu hicho kitaendelea kuwa na umuhimu basi ni sahihi kufanya.

Na swali la tatu ni je kitu hiki kitakuwa na umuhimu kwangu miaka kumi ijayo? Hapa unajiuliza kama miaka kumi kutoka sasa kile ambacho umekwama kufanya kitakuwa na umuhimu kwako.

Kadiri kitu kinavyokuwa na ndiyo kwenye maswali hayo matatu, ndivyo kinavyokuwa muhimu zaidi kwako kufanya. Kama kitu ni muhimu dakika kumi zijazo, lakini miezi kumi ijayo hakina umuhimu, hakipaswi kuwa kipaumbele.

Lakini kama kitu ni muhimu miaka kumi ijayo, lakini siyo muhimu dakika kumi zijazo, kipe kipaumbele kwenye kukifanya.

Jiulize kumi hizo tatu kila unapokwama na utaiona hatua sahihi ya kuchukua.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha