“Were you to live three thousand years, or even a countless multiple of that, keep in mind that no one ever loses a life other than the one they are living, and no one ever lives a life other than the one they are losing. The longest and the shortest life, then, amount to the same, for the present moment lasts the same for all and is all anyone possesses. No one can lose either the past or the future, for how can someone be deprived of what’s not theirs?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 2.14
Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MUDA PEKEE UNAOMILIKI…
Ni muda ulionao sasa, huu ndiyo muda unaomiliki, ndiyo muda unaoweza kuutumia kufanya chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Muda uliopita haupo chini ya umiliki wako, chochote ambacho ulishafanya huwezi kukibadili sasa.
Muda ujao nao haupo kwenye umiliki wako, huwezi kupangilia muda huo kwa uhakika kwa kuwa hujui nini kitakuja na muda huo.
Hivyo tunabaki na muda tulionao sasa, huu ndiyo muda pekee unaoweza kuutumia kufanya mambo yote muhimu ya maisha yako.
Changamoto ni kwamba muda huu haudumu, ni muda unaopita kwa kasi sana.
Hivyo tunapaswa kuutumia muda huu vizuri, kwa kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwenye maisha yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kumiliki muda ulionao sasa, kuutumia kufanya makubwa na kuepuka kuupoteza kwa kufikiria muda uliopita au muda ujao.
Weka nguvu na umakini wako wote kwenye muda ulionao sasa na utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
#MudaNiSasa, #JanaImepita, #KeshoHaijafika, #IshiLeo
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha