“The diseases of the rational soul are long-standing and hardened vices, such as greed and ambition—they have put the soul in a straitjacket and have begun to be permanent evils inside it. To put it briefly, this sickness is an unrelenting distortion of judgment, so things that are only mildly desirable are vigorously sought after.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 75.11

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UGONJWA SUGU WA ROHO…
Ugonjwa sugu wa roho ni tamaa.
Tamaa ikishamtawala mtu, hawezi tena kufikiri kwa umakini,
Tamaa ikishamsukuma kupata kile anachotaka, atatumia njia ambazo hata siyo sahihi ili apate anachotaka.
Na anaweza kupata anachotaka ndani ya muda mfupi, lakini baadaye linakuja anguko ambalo linapelekea apoteze kila alichopata kwa tamaa.

Tunapaswa kujikinga sana na tamaa, chochote tunachofanya, tusiwe watu wa kusukumwa na tamaa.
Tusikazane kupata kitu hata kwa njia zisizo sahihi.
Chochote ambacho kinapatikana kwa njia zisizo sahihi kitaondoka haraka sana na kuacha maumivu makubwa.

Tuzitibu roho zetu kwa kuondokana na hisia za tamaa, hisia za kutaka kupata zaidi ya unavyostahili, hisia za kupata zaidi ya wengine na hisia za kutumia kila njia hata kama siyo sahihi ili tu kutimiza tamaa yako.

Njia sahihi ya kupata unachotaka ni ndefu na inachukua muda, lakini unapopata kitu kwa njia sahihi, unapata ridhiko la roho na hata kinapoondoka hupati maumivu, kwa kuwa unajua utapata tena.
Lakini unapopata kitu kwa tamaa, unakosa kujiamini na kinapopotea unaumia na kukata tamaa kabisa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuondokana na ugonjwa sugu wa roho ambao ni tamaa.
#TamaaNiMbaya, #FanyaKilichoSahihi, #MazuriYanatakaMuda

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha