“Eat like a human being, drink like a human being, dress up, marry, have children, get politically active—suffer abuse, bear with a headstrong brother, father, son, neighbor, or companion. Show us these things so we can see that you truly have learned from the philosophers.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.21.5–6

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KILA KITU NI FALSAFA…
Kila kitu unachofanya kwenye maisha yako ya kila siku, unaweza kukifanya kwa ukawaida au ukakifanya kifalsafa.
Kwa ukawaida ni pale unapofanya kwa mazoea, unapofanya ili kumaliza kufanya na hakuna kipya unachoweka au kujifunza.
Lakini kufanya kitu kifalsafa ni kukifanya kwa utofauti mkubwa, kukifanya kwa upekee kama vile ndiyo mara ya kwanza kufanya na kukifanya kama ndiyo mara ya mwisho kufanya.

Jinsi unavyokula, unavyokunywa, unavyovaa, unavyoendesha mahusiano yakonna wengine, na hata unavyokabiliana nanchangamoto unazokutana nazo, inaonesha kama kweli umeiva kifalsafa au bado.

Kuna falsafa kwenye kila unachofanya, na njia pekee ya kupima uivaji wako wa kifalsafa ni matendo yako, na siyo maneno yako.
Kila unachokifanya, kifanye kwa misingi ya falsafa, hasa falsafa ya ustoa.
Na kamwe hutazoea kitu, utaweza kufanya kitu kwa umakini na ubora na utapata matokeo bora sana.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kila kitu katika misingi ya falsafa.
#IshiKiFalsafa, #MaishaNiUnachofanyaSiyoUnachosema, #UtapimwaKwaMatendoSiyoManeno

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha