“How does your ruling reason manage itself? For in that is the key to everything. Whatever else remains, be it in the power of your choice or not, is but a corpse and smoke.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 12.33
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KINACHOSIMAMIA MISINGI YAKO…
Kuna misingi unayotumia katika kufikiri na kufanya maamuzi.
Swali ni je misingi hii inasimamiwa na kuongozwa na nini?
Bila ya kuwa na kitu kinachosimamia na kuongoza misingi yako, haitakuwa na manufaa kwako.
Ni rahisi kuteleza na hata kujidanganya kama huna kinachosimamia misingi hiyo.
Moja ya changamoto zinazotusumbua ni kushindwa kujidhibiti wenyewe.n
Tunaweza kuwa na mipango mizuri sana na nia njema ya kuitekeleza, na kuwa tayari kuchukua hatua, lakini inapofika wakati wa kuchukua hatua, tunakwamishwa na vitu vidogo vidogo.
Ni lazima tuwe na kitu kinachosimamia misingi yetu, ili tuweze kuiishi bila ya kutetereka.
Kuwa na mfumo bora wa kupima misingi yako na utekelezaji unaofanya ili kuona kama unapiga hatua au umekwama pale pale.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na kitu cha kusimamia misingi unayotumia kufanya maamuzi na kuchukua hatua.
#SimamiaMisingiYako, #Usijidanganye, #PimaHatuaUnazopiga
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha