“Life without a design is erratic. As soon as one is in place, principles become necessary. I think you’ll concede that nothing is more shameful than uncertain and wavering conduct, and beating a cowardly retreat. This will happen in all our affairs unless we remove the faults that seize and detain our spirits, preventing them from pushing forward and making an all-out effort.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 95.46
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TATIZO LA KUKOSA MPANGO…
Maisha bila ya mpango ni majanga,
Unapoanza kufanya kitu bila ya kuweka mpango wowote wa namna gani unaenda kukifanyanna matokeo gani unategemea kupata, umeshashindwa kabla ya kuanza.
Lakini wengi ndivyo wanavyopeleka maisha yao hivi, wanafanya mambo kwa mazoea na kadiri wanavyokutana nayo, hivyo hawapati matokeo mazuri.
Wakati mwingine watu wanafanya mambo bila mpango kwa sababu ya woga na kukosa ujasiri. Mtu anakuwa hajiamini na hayupo tayari kujisukuma kutoa matokeo bora. Hivyo anafanya bila mpango na akipata matokeo mazuri anajiona ana uwezo mkubwa. Akipata matokeo mabovu anajiambia hata hivyo hakuwa na mpango.
Kuendesha maisha bila mpango haina tofauti na mwanafunzi anayeingia kwenye mtihani akiwa hajajisomea vya kutosha. Akibahatisha kufaulu mtihani huo atajiambia ana akili sana.
Lakini ikitokea amefeli mtihani huo, atajiambia hata hivyo hakuwa amesoma.
Unaona hapo jinsi ambavyo mtu anashindwa kujikabili mwenyewe na kukubali uzembe wake uliomwingiza kwenye hali anayojikuta.
Rafiki, usifanye kitu chochote kabla ya kuweka mpango,
Usiianze siku yako kabla hujawa na mpango wa siku nzima.
Usianze kutekeleza jukumu lolote, hata kama ni mazungumzo na mtu mwingine kabla hujajiwekea mpango.
Acha kujidanganya na acha kujikimbia mwenyewe, weka mpango ambao utausimamia na kujipima nao, kama kuna uzembe utauona kirahisi ukiwa na mpango kuliko kufanya kwa mazoea.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na mpango kwenye kila unachokwenda kufanya na kuondoa kabisa mazoea.
#MaishaMipango, #UsijidanganyeMwenyewe, #EpukaMazoea
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha