“Hurry to your own ruling reason, to the reason of the Whole, and to your neighbor’s. To your own mind to make it just; to the mind of the Whole to remember your place in it; and to your neighbor’s mind to learn whether it’s ignorant or of sound knowledge—while recognizing it’s like yours.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.22
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari FIKIRI KWENYE KILA JAMBO…
Kwa kila jambo unalofanya kwenye maisha yako,
Kwa kila maamuzi unayofikia,
Hakikisha umefikiri kwa akili yako mwenyewe.
Usikimbilie kufanya jambo au kufikia maamuzi kwa msukumo wa hisia ambazo umezipata, utafanya maamuzi mabovu ambayo utayajutia sana.
Usifanye jambo kwa sababu ndivyo ambavyo umekuwa unafanya mara zote, jiulize tena na tena kama ndiyo jambo sahihi kufanya na kama unalifanya kwa usahihi.
Pia usifanye jambo kwa sababu ndivyo kila mtu anafanya, kitu hakiwi sahihi kwa sababu kila mtu anafanya. Na mara nyingi kile ambacho kila mtu anafanya huwa siyo kitu sahihi.
Jambo sahihi kufanya, maamuzi sahihi kwako ni yale ambayo wewe mwenyewe umeyafikiria kwa akili yako na ukiwa na utulivu wa akili.
Akili yako inajua mengi sana kama utaipa nafasi ya kufikiri kwa uhuru, bila ya kuelemewa na hisia ambazo unakuwa umejiwekea.
Fikiri kwa utulivu, umakini na usahihi kwa kila jambo,
Ondoa hisia na weka mazoea pembeni,
Na hapo akili yako itakupa nguvu kubwa ya kuona kile ambacho ni sahihi kwako kufanya.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufikiri kwa usahihi kila unachofanya na siyo kufanya kwa mazoea au kusukumwa na hisia.
#FikiriKwaUsahihi, #DhibitiHisiaZako, #AchanaNaMazoea
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani ,
http://www.amkamtanzania.com/kocha