“When you first rise in the morning tell yourself: I will encounter busybodies, ingrates, egomaniacs, liars, the jealous and cranks. They are all stricken with these afflictions because they don’t know the difference between good and evil. Because I have understood the beauty of good and the ugliness of evil, I know that these wrong-doers are still akin to me . . . and that none can do me harm, or implicate me in ugliness—nor can I be angry at my relatives or hate them. For we are made for cooperation.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 2.1
Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIANDAE KWA USIYOTEGEMEA…
Huwa tunazianza siku zetu tukiwa na mipango mikubwa na mizuri kwenye siku hiyo.
Tunapangilia kila kitu na kupata picha mambo yakiwa yanakwenda vizuri kabisa.
Lakini kama waswahili wanavyosema, mipango siyo matumizi.
Siku yetu inapoanza, ndipo tunakumbana na uhalisia ambao hatukuutegemea kwenye mipango yetu.
Tunakutana na watu ambao wanatukwaza na kutukwamisha, wanatuchelewesha kukamilisha kile tulichopanga.
Tunakutana na wengine ambao wanataka kutumia kazi zetu kwa manufaa yao.
Na pia wapo watakaokusema vibaya wakati hakuna chochote kibaya umefanya.
Watu wa aina hii wana nguvu kubwa ya kuvuruga siku zetu kama hatujajipanga vizuri.
Hivyo tunapaswa kujipanga vizuri tunapoianza siku yetu, kwa kujiandaa na tusiyotegemea.
Ili sasa unapokutaha na haya, unapokutana na watu wa aina hiyo, moyoni unajiambia nilijua nitakutana na mtu kama wewe, lakini huwezi kuniyumbisha, mipango yangu inaendelea kama nilivyopanga.
Kauli hiyo ina nguvu kubwa kwako kuendelea kuliko kukutana na hali kama hizo ukiwa huna matarajio wala maandalizi.
Ukawe na siku bora sana leo, siku ya kujiandaa kwa usiyotegemea na kuwa tayari kuwashinda wale watu wenye hila za kukuzuia usipige hatua.
#UsiyotegemeaYatatokea, #WenyeHilaWanakuwinda, #KilaSikuNiVita
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha