“First tell yourself what kind of person you want to be, then do what you have to do. For in nearly every pursuit we see this to be the case. Those in athletic pursuit first choose the sport they want, and then do that work.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.23.1–2a

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUWA MTU UNAYETAKA KUWA…
Kila mtu anatamani kuwa mtu wa aina fulani, mtu wa mafanikio, lakini ni wachache sana wanaofikia matamanio hayo.
Hii ni kwa sababu wengi huishia kwenye matamanio, hawaendi kwenye kuchukua hatua za kuyafanya matamanio hayo kuwa uhalisia.

Kwanza kabisa unapaswa kujiambia unataka kuwa mtu wa aina gani, kisha kujua ni vitu gani unapaswa kufanya ili kuweza kuwa mtu wa aina hiyo kweli.
Ukishajua unachopaswa kufanya ili kuwa mtu unayepaswa kuwa, chukua hatua, weka kazi ili kuweza kufikia vile unavyotaka kuwa.

Hakuna aliyewahi kuamka asubuhi akajikuta ni mchezaji bora, bali kila mchezaji bora ameweka miaka mingi ya kufanya mazoezi na kujiboresha zaidi.
Hakuna aliyewahi kuamka asubuhi na kujikuta ana mafanikio makubwa, bali mafanikio yamekuwa yanatengenezwa kwa hayua ndogo ndogo mtu anazopiga kila siku.

Usitegemee njia ya mkato katika kuwa mtu unayetaka kuwa, bali kuwa tayari kuweka kazi ili kuwa vile unavyotaka kuwa.
Pia jipe muda kufikia vile unavyotaka kuwa, maana haraka na kukosa subira itakupelekea kufanya maamuzi mabovu kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujua unataka kuwa mtu wa aina gani, kisha kuweka kazi ili kuweza kuwa mtu huyo.
#MaishaNiKuchagua, #UnawezaKuwaUtakavyo, #KaziHaikwepeki

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha