“Then what makes a beautiful human being? Isn’t it the presence of human excellence? Young friend, if you wish to be beautiful, then work diligently at human excellence. And what is that? Observe those whom you praise without prejudice. The just or the unjust? The just. The even-tempered or the undisciplined? The even-tempered. The self-controlled or the uncontrolled? The self-controlled. In making yourself that kind of person, you will become beautiful—but to the extent you ignore these qualities, you’ll be ugly, even if you use every trick in the book to appear beautiful.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.1.6b–9
Ni siku nyingine nzuri, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata fursa nyingine bora kwetu kwenda kuweks juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UZURI WA MTU NI TABIA…
Dunia inaonekana kupima uzuri wa watu kwa vitu mbalimbali, sura, umbo, utajiri, mvuto na kadhalika.
Lakini hebu jiuliza, unapokuwa wewe mwenyewe, ni kitu gani hasa kinakuvutia kwa wale ambao unaona ni wazuri?
Je ni mwonekano au tabia walizonazo?
Kama utakuwa mkweli kwako, jibu ni unavutiwa na watu siyo kwa sababu ya mwonekano wao, bali kwa sababu ya tabia zao.
Unavutiwa na wale ambao wameweza kujijengea nidhamu bora kwenye maisha yao na siyo wale wanaoendeshwa na hisia zao.
Unavutiwa na wale wanaotenda haki na siyo wadhalimu.
Unavutiwa na watu wenye utulivu na siyo wanaowaka hasira kila mara.
Haijalishi mtu ana mwonekano mzuri kiasi gani, kama tabia zake siyo bora hutavutiwa naye.
Hivyo rafiki, kama unataka kuwa mzuri, kama unataka kuwavutia wengine, kazi yako ni moja, kuwa na tabia nzuri, kuwa mtu bora kabisa kwa kufanya kilicho sahihi mara zote.
Hata kama watu hawatakuambia, ndani ya mioyo yao watakubaliana na wewe, watavutiwa na wewe na watakuwa tayari kushirikiana na wewe.
Achana na dunia inayodanganya watu uzuri uko kwenye mwonekano, umbo, sura, vipodozi na mengine ya nje.
Wewe weka juhudi kutengeneza tabia bora na utakuwa mzuri sana kwa wengine, bila ya kujali mwonekano wako wa nje ukoje.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujenga uzuri wako kwa kuwa na tabia bora kabisa.
#UzuriWaMtuNiTabia, #JijengeeTabiaBora, #FanyaKilichoSahihiMaraZote
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha