“Every habit and capability is confirmed and grows in its corresponding actions, walking by walking, and running by running . . . therefore, if you want to do something make a habit of it, if you don’t want to do that, don’t, but make a habit of something else instead. The same principle is at work in our state of mind. When you get angry, you’ve not only experienced that evil, but you’ve also reinforced a bad habit, adding fuel to the fire.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.18.1–5

Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAZOEA HUJENGA TABIA…
Sisi binadamu ni viumbe ww tabia,
Tunapoanza kufanya kitu huwa kinakuwa kigumu kwetu,
Lakini tunapoendelea kufanya, akili yetu inakigeuza kuwa tabia.
Na kitu kikishakuwa tabia, tunaweza kufanya bika hata ya kufikiri.

Hii ina maana kwamba kama kuna tabia unataja kujijengea, basi rudia rudia kufanya kitu hicho mpaka kitakuwa tabia chenyewe.
Kama unataka kuwa na tabia ya kuamka mapema, anza kuamka mapema kila siku na endelea kurudia hilo.
Kama unataka kujijengea tabia ya kujisomea, tenga muda na usome kila siku bila ya kuacha.
Muhimu ni urudierudie kufanya mpaka akili yako ipate ujumbe kwamba kitu hiki ni muhimu na inapaswa kukiweka kwenye tabia.

Upande wa pili wa hili pia ni muhimu.
Kama kuna tabia ambayo unayo sasa na siyo nzuri kwako hivyo unataka uibadilishe, utaibadilisha kwa kutengeneza tabia nyingine mpya.
Usikazane kubadili tabia kwa kutaka kuifuta. Njia pekee ya kubadili tabia ni kutengeneza tabia mpya ya kushika nafasi ya tabia hiyo ya zamani.
Unaootengeneza tabia mpya, unaondoa mazoea kwenye tabia ya zamani na hivyo inakosa nguvu na kupotea yenyewe.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea tabia mpya kwa kutengeneza mazoea yanayojirudia.
#MazoeaHuzaaTabia, #WeweNiKileUnachofanya, #UnajengaTabiaNaTabiaZinakujenga

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha